Klabu ya Sporting CP imeafikia kumfuta kazi kocha Joao Pereira wiki chache baada ya kocha huyo kumrithi Ruben Amorim aliyehamia Uingereza kuongoza Manchester United.
Kufutwa kazi kwa kocha Joao Pereira kunajiri kutokana na matokeo mabovu ambayo klabu ya Sporting CP imekosa kuandikisha tangu kuondoka kwa Amorim.
Awali kabla ya kujiunga na Manchester United kocha Ruben Amorim, alishinda mechi 11 za mwanzo wa msimu kwa faida ya Sporting CP, mojawapo wa sababu zilizofanya Man United kutaka huduma zake na hatimaye kuzipata.
Mtindo huo uliowekwa na Amorim katika Sporting CP, umekosa kulindwa na kocha Joao Pereira ambaye kwa mujibu wa wakala wa soka Fabrizio Romano, usimamizi wa Sporting CP umekatisha mkataba baina yake na Pereira.
Romano kwenye akaunti yake ya Telegram amesema uamuzi wa kumfuta Pereira ulifanywa Jumatatu na kocha huyo anatarajiwa kuondoka klabuni hapo.
“Uamuzi umefanya leo. Joao Pereira ataondoka klabuni hapo.” Aliandika Fabrizio Romano.
Katika mechi nne za ligi ambazo Pereira ameongoza Sporting CP, tangu kuanza rasmi kuongoza klabu hiyo, ameshinda mechi moja pekee.
Kufikia sasa baada ya raundi 15 za ligi ya Liga Portugal,
Sporting CP wanasalia katika nafasi ya pili kwa alama 37, alama moja nyuma ya
viongozi wa ligi hiyo Benfica.
Pereira amepoteza mechi mbili na kutoka sare mechi moja akiwa na Sporting CP.
Mkataba wa Joao Pereira na Sporting CP unakatikachini ya miezi miwili licha ya kuwa ulistahili kukamilika mwaka wa 2027.