logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Barcelona yafuzu fainali ya Spanish Super cup

Mabao ya Gavi na Lamine Yamal yaliiwezesha Barcelona kupata ushindi ya 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao katika nusu fainali.

image
na OTIENO TONNY

Football09 January 2025 - 12:58

Muhtasari




    Mabao ya Gavi na Lamine Yamal yaliiwezesha Barcelona kupata ushindi ya 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao katika nusu fainali ya Spanish Super Cup mjini Jeddah Jumatano na kutinga fainali yao ya tatu mfululizo.

    Gavi alitangulia kufunga dakika ya 17 na Yamal akaifungia Barca bao la pili dakika saba baada ya mapumziko. Barcelona walipata ushindi licha ya kukosekana kwa mchezaji wao Dani Olmo ambaye leseni yake ya kucheza ilifutwa.

    Uamuzi wa Jumatano wa baraza la kitaifa la michezo la Uhispania (CSD) kuruhusu Barcelona kuwasajili kwa muda Dani Olmo na Pau Víctor ulikuja kuchelewa sana kwa mchezo dhidi ya Athletic, lakini wawili hao sasa watapatikana kucheza katika fainali ya Jumapili.

    Barcelona, ​​timu iliyofanikiwa zaidi katika Kombe la Super Cup ikiwa na vikombe 14, itamenyana na washindi wa nusu fainali ya Alhamisi kati ya Real Madrid na Mallorca katika fainali siku ya Jumapili.

    Mabingwa wa Uhispania na Ulaya Real Madrid watamenyana na washindi wa pili wa kombe la Mallorca siku ya Alhamisi katika nusu fainali ya pili nchini Saudi Arabia, ambapo mashindano hayo yamekuwa yakiandaliwa  kwa miaka michache iliyopita.

    Yamal akihojiwa baada ya mechi hiyo alikiri kwamba timu ya Athletic ni timu ngumu na inahitaji wapinzani wenye mbio kali ili kuwadhibiti.

    "Athletic ni timu ya kutumia nguvu na mwili ambayo inakufanya kukimbia sana, tuliteseka zaidi ya yote hadi mwisho, lakini tuliweza kucheza vizuri na tuna furaha sana," Yamal aliiambia Movistar.

    Kocha wa Barca Hansi Flick alipongeza uamuzi wa baraza la kitaifa la michezo la Uhispania kuhusu Olmo na Victor.

    ‘’Klabu nzima ina furaha kubwa kwa uamuzi huu sahihi,’’ Alisema Flick.

    Macho yote sasa yatakuwa yanaangazia matokeo ya mchuano kati ya Real Madrid na Malloca ambayo inakaragazwa Alhamisi 9, Januari 2025. Huku timu yenye itafuzu ndio itamenyana na Barcelona katika fainali Jumapili.



    RADIO JAMBO FREQUENCIES

    Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


    logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved