Timu ya soka ya Kenya Harambee Stars wanamatumaini ya kufika
katika fainali ya kinyang’anyiro ya kombe la Mapinduzi. Stars wanahitaji
matokeo ya sare katika mechi yao ya mwisho katika kikundu dhidi ya wenyeji wa
mashindano hayo Zanzibar .
Iwapo mchuano huo ambapo utakaragazwa katika uga wa Gombani Ijumaa kuanzia saa moja jioni itaishia sare basi Harambee stars watafuzu moja kwa moja hadi katika fainali ya kombe la Mapinduzi.
Harambee Stars kwa sasa wanashikilia nafasi ya kwanza na pointi 4 huku Burkina Faso wanafuata kwa karibu na pointi 4 huku Kenya wakiwa mbele na idadi ya mabao, Timu ya Zanziba wanashikilia nafasi ya tatu na pointi tatu huku Tanzania wakishikilia nafasi ya mwisho ikiwa hawajaandikisha pointi yeyote.
Kati ya mechi mbili ambazo zimekaragazwa tayari timu ya Kenya imetua ushindi katika mechi moja waliocheza dhidi ya Tanzania walipoilaza mabao mawili kwa nunge na kuenda sare ya bao moja na timu ya Bukina Faso.
Mechi hiyo kati ya Kenya na Zanzibar itaamua hatma ya Kenya kwani wanahitaji ushindi au sare ili kufuzu fainali .
Timu mbili ambazo zitamaliza katika nafasi ya kwanza na ya pili mtawalia zitafuzu kushiriki fainali ambayo imeratibiwa kukaragazwa tarehe 13, January
Michuano ya Mapinduzi Cup inaipa Kenya fursa nzuri ya kufanya maandalizi mazuri kabla ya michuano ijayo ya CHAN, ambayo itaandaliwa nchi tatu za Africa Mashariki ikiwemo Kenya, Uganda na Tanzania baadaye mwaka huu.