Ligi kuu ya soka nchini Kenya FKFPL inarejea wikendi hii kwa muendelezo wa mechi za msimu huu wa 2024/2025, jumla ya mechi sita zikiratibiwa kuchezwa kati ya Jumamosi na Jumapili. Mechi tatu zitachezwa Jumamosi na nyingine tatu kuchezwa Jumapili mtawalia.
Kwenye ratiba iliyopangwa kuchezwa wikendi hii, Posta Rangers watakuwa nyumbani ugani Machakos kuwaalika Nairobi City Stars mwendo wa saa saba mchana. Baada ya kukamilika kwa mechi ugani hapo, mwendo wa saa kumi jioni itakuwa zamu ya Kakamega Homeboyz kutoka magharibi wakapoalikwa na FC Talanta.
Jumamosi hiyo, mechi itakayoangaziwa Zaidi na mashabiki wa soka nchini itawaleta pamoja Shabana FC na Tusker FC katika uwanja wa Gusii kuanzia saa nane mchana.
Jumapili itakuwa zamu ya wanajeshi Ulinzi Stars watakomenyana na timu ya Mara Sugar katika uwanja wa Dandora jijini Niarobi kuanzia saa saba mchana. Bidco United watakuwa wenyeji wa Murang’a Seal kutoka maeneo ya kati ya Kenya katika uwanja wa Machakos kuanzia saa tisa mchana.
Mechi ya mwisho itachezwa ugani Dandora kuanzia saa kumi jioni ambapo Mathare United watawaalika Kariobangi Sharks.
Ligi hiyo ilihairishwa mechi za wikendi iliyopita kutokana na mabadiliko ya ofisini yanayofanywa na uongozi mpya uliochagulia mnamo Disemba 7 katika uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka nchini.
Kufikia raundi ya 15 ya msimu huu KCB inaongoza msimamo wa
jedwali ikibanana alama na Tusker. Wote wana alama 27 baada ya michuano 15 ya
ligi.