Kiungo cha kati katika timu ya Manchester United Kobbie Mainoo na winga Alejandro Garnacho huenda watasalia kambini Old Trafford licha ya hatari ya Manchetser United kukabiliwa na vitisho vya ukiukaji wa kanuni za faida na uendelevu.
Kwa mujibu wa kanuni za faida na uendelevu (PSR) vilabu vya soka vinastahili kuwaachilia wachezaji wa soka ambao wamelelewa klabuni hapo kuanzia kwenye academia hadi kwenye timu kuu. Katika msimu huu Manchester United haijawaachilia wachezaji amabo wamekuzwa na klabu hiyo na wanastahili kufanya hivo katika kipindi hiki cha uhamisho wa majira ya baridi.
Katika timu hiyo, Mainoo, Marcus Rashford na Garnacho ni baadhi ya wachezaji ambao wamekuzwa klabu hiyo.
Kwa mujibu wa Sky Sports, Kobbie Mainoo amekuwa kwenye mazungumzo kuhusu mpango mpya na ulioboreshwa, wakati Garnacho pia yuko katika mipango ya Ruben Amorim. Sky Sports imeripoti kuwa lengo la Manchester United ni kuhamisha wachezaji ambao hawaendani na muundo wa meneja.
Mkataba wa Mainoo na Man United unatarajiwa kukamilika mwaka wa 2027 ila una kipengee cha kuongezwa mwaka mmoja ikiwa ataridhisha klabu hiyo. Kwa upande wa Garnacho, mkataba wake na klabu hiyo unatarajiwa kukamilika mwaka wa 2028.
Kulingana na kanuni za PSR, klabu inastahili kuwauza wachezaji wake iliyowalea na kuunda jumla ya angalau pauni milioni sabini katika mauzo hayo kila msimu.
Ikiwa kanuni hiyo haitazingatiwa, klabu itazuiwa kufanya usajili na kuuza wachezaji wake kwa muda wa angalau miaka miwili na mamlaka husika.
Mbali na hatma ya Mainoo na Garnacho, Man United pia
kulingana na jarida la Independent, inahitajika kufanmya mauzo ili kuafikia
Yuro milioni 60 ili kupata usajili wa Mreno Nuno Mendes mwenye umri wa miaka 22
kutoka Paris Saint-Germain.