Mabingwa wa Uhispania Real Madrid watachuana na Barcelona
katika fainali ya Spanish Super Cup Jumapili tarehe 12, January 2025.
Real Madrid iliicharaza timu ya Malloca siku ya Alhamisi katika nusu fainali mabao matatu kwa sufuri huku awali Barcelona iliicharaza Athletic Bilbao mabao mawili kwa sufuri na kuwapa nafasi ya kufuzu moja kwa moja kwa fainali ya Spanish Super Cup.
Jude Bellingham na Rodrygo walipachika mabao na kuipa Real Madrid ushindi uliowawezesha kufuzu kushiriki fainali na wapinzani wao wa jadi Barcelona.
Madrid wana nafasi ya kulipiza kisasi kwa kushindwa kwao kwa Clasico katika La Liga mwezi Oktoba 2024, ambapo Barcelona ilipata ushindi wa 4-0 dhidi yao.
Mashabiki wa Madrid walijaza uga wa Jeddah kuishabikia timu yao ambayo ilionekana kutumia vizuri nafasi walizozipata kwa faida yao huku bao la kujifunga lake Valjent likifanikisha ushindi pamoja na bao la tatu kutoka kwa mchezaji Rodrygo katika dakika za lala salama.
Wapenzi wa soka sasa wanatarajia kushuhudia fainali hiyo ambayo itachezwa katika uga wa King Abdullah Sports City.