Shabiki huyo mdogo wa timu
ya Newcastle United alionekana kwenye televisheni wakati wa mechi wa
Newcastle dhidi ya Arsenal ambapo Newcastle ilipata ushindi ya 2-0.
Shabiki huyo anayejulikana kama Sammy alionekana kwenye mitandao ya kijamii akisherehekea baada ya mechi kukamilika kule Kaskazini mwa London katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Carabao.
Sammy Scott alikuwa na hamu ya kuona nusu ya Kombe la Carabao akiwa na baba yake Mark kwa hivyo mama yake Claire aliiambia shule yake kwamba alikuwa mgonjwa.
Lakini walitua kwenye maji moto wakati kamera za Sky zilipomchagua Sammy aliyekuwa akishangilia akikunja ngumi na kupiga mayowe ya furaha baada ya Anthony Gordon kunyakua mshindi katika ushindi wa 2-0.
Matangazo ya moja kwa moja yalinasa hisia zake za furaha, ambazo zilisambaa haraka kwenye mitandao ya kijamii. Kwa bahati mbaya kwa shabiki huyo mchanga, picha hizo pia zilifikia usimamizi wa shule yake.
Muda mfupi baada ya mechi, wazazi wake walipokea barua rasmi kutoka kwa usimamizi wa shule hiyo ikisema kuwa kukosa kwa Sammy shuleni itachukuliwa kama kukosa shule bila ruhusa.
‘’ Wazazi wapendwa, tungependa kukufahamisha kuwa kutokuwepo kwa Sammys shuleni kuanzia Jumanne tarehe 7 Januari kutachukuliwa kuwa bila idhini .Hii ni kutokana na kanda iliyosambaa kwenye vyombo vya habari inayomuonyesha Sammy akiwa mbali na London kwenye mechi ya soka.Tafadhali wasiliana nasi shuleni ikiwa ungependa kujadili hili zaidi’’ Hii ni kutokana na barua iliyoandikwa na usimamizi wa shule hiyo.
Picha za shabiki huyo mchanga zimesambaa mtandaoni.