logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Alexander Isak achaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi EPL, Northingham ikichukua kocha bora

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alimshinda mwenzake Jacob Murphy, ambaye pia aliorodheshwa kwenye tuzo hiyo

image
na OTIENO TONNY

Football11 January 2025 - 07:54

Muhtasari


  • Isak pia aliorodheshwa na kushinda tuzo la bao bora la mwezi la Guinness.
  • Isak ndiye mchezaji wa kwanza wa Uswidi kushinda tuzo ya Goli Bora la Mwezi la Guinness tangu ilipoanzishwa 2016/17.


Mshambulizi wa Newcastle United Alexander Isak amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa mwezi Disemba.

Mchezaji huyo wa mbele wa Uswidi alikuwa katika kiwango cha hali ya juu mwezi wa mwisho wa 2024, akifunga mabao manane ikiwa  bao zuri dhidi ya Liverpool, moja dhidi ya Brentford, lingine dhidi ya Leicester City, bao la kwanza la Magpies dhidi ya Ipswich Town, moja dhidi ya Aston Villa na bao la kwanza la ufunguzi dhidi ya Manchester United pamoja na kusajili pasi mbili za mabao.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alimshinda mwenzake Jacob Murphy, ambaye pia aliorodheshwa kwenye tuzo hiyo pamoja na wachezaji wawili wa Liverpool Trent Alexander-Arnold na Mohamed Salah, Morgan Gibbs-White wa Nottingham Forest, Dean Huijsen wa AFC Bournemouth, Cole Palmer wa Chelsea na Antonee Robinson wa Fulham.

Isak pia aliorodheshwa na kushinda tuzo la bao bora la mwezi la Guinness kufuatia uchezaji wake wa ajabu wa umbali wa yadi 20 wakati wa sare ya kusisimua ya 3-3 dhidi ya viongozi wa ligi ya premia Liverpool.

Isak ndiye mchezaji wa kwanza wa Uswidi kushinda tuzo ya Goli Bora la Mwezi la Guinness tangu ilipoanzishwa 2016/17, na mchezaji wa kwanza wa Newcastle kufanya hivyo tangu Almiron mnamo Oktoba 2022.

Mshambuliaji huyo wa Newcastle  amekuwa mchezaji wa nne wa Uswidi kushinda tuzo hiyo akimfuata Freddie Ljungberg akiwa Arsenal mnamo Aprili 2002, Johan Elmander akiwa Bolton Wanderers mnamo Novemba 2010, na Zlatan Ibrahimovic akiwa Manchester United mnamo Desemba 2016.

Yeye ni mmoja wa wachezaji sita pekee walioshinda tuzo zote mbili kwa mwezi mmoja, akifuata Cole Palmer aliyeshinda tuzo hizo mbili mnamo Aprili 2024, Bruno Fernandes mnamo Juni 2020, Jesse Lingard mnamo Aprili 2021, Mohamed Salah mnamo Oktoba 2021 na Miguel Almiron mnamo Oktoba 2022.

Kocha wa timu ya Nottingham Forest Nuno Espirito kwa mara ya pili msimu huu, Nuno Espírito Santo ametunukiwa tuzo ya meneja bora wa mwezi wa ligi kuu ya Uingereza.

Baada ya kushinda mechi  tano kati ya sita mwezi Desemba, kipindi hicho cha sherehe kimekuwa cha mafanikio kwa Klabu hiyo ya Forest  huku  Nuno sasa anakuwa meneja wa kwanza kushinda tuzo hiyo mara mbili katika kampeni ya sasa.

Nuno amesisitiza umuhimu wa kusimamia michezo, kutafuta njia tofauti za kushinda katika hali zote, na ari ya pamoja pia imeangaziwa kuwa muhimu katika hali nzuri kufikia sasa

Mbio za ushindi za Forest  zilianza Old Trafford, kwa mabao ya Nikola Milenković, Morgan Gibbs-White, na Chris Wood yakiipa timu hiyo ushindi mnono ugenini dhidi ya Manchester United.




 



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved