logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harambee Stars kujua wapinzani wao katika mashindano ya CHAN 2025

Harambee Stars itajua wapinzani wao katika kundi lao la kufuzu kwa CHAN 2025 katika hafla itakayoandaliwa 15 Januari katika ukumbi wa KICC Nairobi

image
na OTIENO TONNY

Football15 January 2025 - 11:29

Muhtasari


  • Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limepanga kuandaa droo ya michuano ya mataifa ya Afrika ya TotalEnergies Africa (CHAN).
  • Kenya, pamoja na Uganda na Tanzania, zitashiriki michuano ya kufuzu kwa kanda ya CECAFA ikiwa ni  wao ndio watakuwa waandalizi wa michezo hizo.


Harambee Stars itajua wapinzani wao katika kundi lao la kufuzu kwa CHAN 2025 katika hafla itakayoandaliwa 15 Januari katika ukumbi wa KICC Nairobi kuanzia saa mbili usiku, huku Kenya ikijiandaa kuandaa mchuano huo.

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limepanga kuandaa droo ya michuano ya mataifa ya Afrika ya TotalEnergies Africa (CHAN) .

Tukio hili linatarajiwa kubainisha makundi ya michuano hiyo itakayoandaliwa kwa pamoja kati ya Kenya, Uganda na Tanzania.

Kenya, pamoja na Uganda na Tanzania, zitashiriki michuano ya kufuzu kwa kanda ya CECAFA ikiwa ni  wao ndio watakuwa waandalizi wa michezo hizo.

Kenya, Tanzania, Uganda, Morocco, Guinea, Senegal, Mauritania, Niger, Burkina Faso, Nigeria, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kongo, Sudan, Zambia, Angola na Madagascar ni miongoni mwa timu zilizofuzu kushiriki CHAN.

Droo hiyo ni muhimu kwa timu zote zitakazoshiriki kwani inaweka mazingira mazuri ya kushiriki katika mashindano hayo, ambapo ni wachezaji wa ligi za ndani pekee wanaruhusiwa kuwakilisha nchi zao.

Mashabiki na viongozi wa  kandanda kote barani humu wanasubiri kwa hamu matokeo hayo ambayo itachagiza mkondo wa michuano hiyo na kuelekea kwenye kutambua mabingwa wa kandanda barani Afrika

Droo ya leo huenda ikashirikisha timu 17 ambazo tayari zimefuzu, Hapo awali, timu 19 zililengwa kushiriki  huku mshindi wa taji hilo kwa sasa ni Senegal.

Tukio hilo linakuja siku moja baada ya bodi hiyo kutangaza kuahirishwa kwa mashindano hayo kutoka Februari hadi Agosti kwa sababu ya changamoto  ya miundombinu hasa yanayotokana na ukarabati ambao unaendelea katika uga mbalimbali ikiwemo uga ya Kasarani sports Centre.

‘’Wataalamu hao wa ufundi na miundombinu wa shirikisho la soka Afrika (CAF) ambao baadhi yao wamejikita nchini Kenya, Tanzania na Uganda, wameishauri CAF kuwa muda zaidi unaitajika kuhakikisha miundombinu na vifaa vinakuwa katika viwango vinavyohitajika ili kuandaa mashindano ya CHAN,’’ Alisema rais wa CAF Patrice Motsepe.

Hii ni mara ya pili kwa michezo hiyo kuahirishwa. CHAN 2024 awali ilikuwa imepangwa kufanyika Septemba 2024 lakini ilisogezwa hadi kati ya Februari 1 na 28, 2025, kutokana na ukosefu wa viwanja vya mechi vinavyokidhi viwango katika baadhi ya nchi waandalizi, ikiwa ni pamoja na Kenya.

Magwiji watatu wa soka kutoka Kenya, Uganda, na Tanzania wamethibitishwa kushiriki sherehe hizo. Wakiwemo McDonald Mariga wa Kenya, Hassan Wasswa wa Uganda na Mrisho Ngasa wa Tanzania hii ikiwa ni  droo ya makala ya nane ya shindano hilo.

Wasswa, Ngasa, na Mariga ambaye ni makamu wa rais wa FKF kwa sasa nchini Kenya na wenzake wametoa mchango nmkubwa katika ukuaji wa soka barani Afrika na kuleta mchango mkubwa vilevile katika nchi yao.

Wasanii ambao wanatarajiwa kutumbuiza watu wakati wa hafla hiyo ni pamoja na Bien wa Kenya, kikundi cha densi cha Uganda, Ghetto Kids na wanakwaya wa Kenya Kenya’s Own Red Choir.


 



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved