logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Garnacho bado anajifunza kucheza katika mfumo wangu mpya – Ruben Amorim

Ruben Amorim ametoa taarifa za ukweli na uwazi kuhusu mustakabali wa Alejandro Garnacho katika klabu ya Manchester.

image
na OTIENO TONNY

Football16 January 2025 - 15:16

Muhtasari


  • Mchezaji huyo wa taifa la Argentina alijitambulisha kama winga mkali katika kikosi cha the Reds baada ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza chini ya mkufunzi Erik Ten Hag.
  •  Mkufunzi huyo wa Manchester anatekeleza falsafa yake Old Trafford, ambayo inahusisha kikosi cha kwanza cha United kuzoea mtindo tofauti kabisa wa soka.


Ruben Amorim anasema Alejandro Garnacho anaimarika nyuma ya pazia anapojifunza kucheza katika mfumo mpya ambao ameleta katika kikosi hicho cha United.

Mchezaji huyo wa taifa la Argentina alijitambulisha kama winga mkali katika kikosi cha the Reds baada ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza chini ya mkufunzi Erik Ten Hag mnamo mwaka wa 2022.

Mkufunzi huyo wa Manchester anatekeleza falsafa yake Old Trafford, ambayo inahusisha kikosi cha kwanza cha United kuzoea mtindo tofauti kabisa wa soka.

Ruben alikiri kuwa anajua itachukua muda kwa baadhi ya wachezaji kuzoeas mfumo huo mpya wa mchezo akiwemo Garnacho na ndio maana anaimani kuwa Garnacho bado ana mustakabali katika klabu hiyo licha ya uvumi unaoendelea kuhusu kuhamia Serie A.

‘’Anahitaji kucheza vizuri zaidi ndani, anaboresha nafasi yake wakati hana mpira. Lakini kwa kufanya hivyo, wakati mwingine hayuko mahali pazuri pa kufanya mabadiliko kama alivyokuwa zamani kwa sababu napenda kulinda na kisha kujenga upya na timu yote ili kufikia awamu ya tatu ya mwisho,’’ Hii ni kutokana na ujumbe aliotoa Amorim.

Amorim anaonyesha kuwa ana subira na mchezaji Garnacho na kwamba anamwaminia.

‘’Anatafuta njia bora ya kucheza katika mfumo huu. Anajiboresha wakati wa mazoezi , alianza katika mchezo uliopita wacha tuone kesho wakati tutacheza na Southampton’’ Aliongeza Amorim.

Siku Manchester United ilipiga Arsenal kwa mikwaju ya penalti Jumapili katika mechi ya raundi ya tatu ya kombe la FA ndio ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Garnacho kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Amorim tangu United iliposhindwa 3-2 na Nottingham Forest Disemba mwaka jana.

Timu ya PSG ilionesha nia ya kumsajili Garnacho ila sasa wako mbioni kumsajili Khvicha Kvaratskhelia kutoka Napoli. Dili hiyo imeibua ripoti kuwa Napoli ipo tayari kutoa kima cha dola milioni 38 hii wiki ili kumsaini Garnacho ambaye atachukua nafasi yake nyota huyo wa Georgia.

Gazeti la Independence linadai kwamba Napoli wanafanya dili na Garnacho anasemekana kuwa tayari kuchukua hatua ambayo ikifaulu itamfanya kujiunga na mchezaji mwenzake wa zamani Scott Mc Tominay ambaye nyota yake inaendelea kung’aa Italia.

Marcus Rashford aliachwa nje ya kikosi ya United wakati walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester City. Mchezaji huyo ambaye amekuwa akihusishwa na fununu ya kutaka kuondoka Man United amekuwa akikosa katika kikosi katika wiki zilizopita kutokana na Kuugua.

sasa watu wanaangazia  iwapo Rashford ataitwa kwenye kikosi kitakachomenyana na Southampton kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved