logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wachezaji wa Arsenal wamfariji Jesus kwa njia maalum huku Arteta akithibitisha atakuwa nje muda mrefu

kocha Mikel Arteta alithibitisha kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 atakuwa nje kwa muda mrefu.

image
na Samuel Mainajournalist

Football16 January 2025 - 08:18

Muhtasari


  • Wachezaji wa Arsenal walimuonyesha upendo na kumfariji mchezaji mwenzao Gabriel Jesus aliyejeruhiwa kwa kuvaa jezi zenye jina lake mgongoni kabla ya mechi yao ya London Derby.
  •  Arteta alithibitisha kuwa kilabu hicho cha kinatafuta kuimarisha safu ya ushambuliaji kwani Bukayo Saka pia atakuwa nje kwa miezi kadhaa.


Wachezaji wa Arsenal walimuonyesha upendo na kumfariji mchezaji mwenzao Gabriel Jesus aliyejeruhiwa kwa kuvaa jezi zenye jina lake mgongoni kabla ya mechi yao ya London Derby dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Mbrazil huyo alitolewa nje kwa machela wakati Arsenal ilipopoteza mchuano wa Kombe la FA dhidi ya Manchester United wikendi, na ikathibitishwa baadaye kuwa fowadi huyo alikuwa na jeraha la anterior cruciate ligament.

Kabla ya mechi ya debi ya London kaskazini Jumatano, wachezaji wa Arsenal walivaa jezi maalum za ukumbusho, hata licha ya kukejeliwa awali kwa kupanga kufanya hivyo kwa ajili ya mchezaji huyo wa miaka 27.

Vijana wa kocha Mikel Arteta walivalia jezi zenye jina "G. Jesus" na nambari yake ya kikosi nambari tisa kabla ya mechi iliyochezwa katika uwanja wa Emirates Jumatano usiku. Sehemu ya juu ya shati pia ilikuwa na ujumbe uliosomeka: "Simama imara Gabby".

Inabakia kuonekana ni muda gani Jesus atakuwa nje akiwa amejeruhiwa. Baada ya mechi ya Tottenham, Arsenal watawakaribisha Aston Villa katika mechi ya Ligi ya Premia siku ya Jumamosi.

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa mchuano huo, kocha Mikel Arteta alithibitisha kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 atakuwa nje kwa muda mrefu.

Wakati huo huo, alithibitisha kuwa kilabu hicho cha kinatafuta kuimarisha safu ya ushambuliaji kwani Bukayo Saka pia atakuwa nje kwa miezi kadhaa.

"Kwa hakika tutajaribu sokoni na tunataka kuimarisha mashambulizi. Tumepoteza wachezaji wawili wakubwa, Bukayo kwa muda wa miezi 3 na Gabriel Jesus atakuwa nje kwa muda mrefu,” Arteta aliambia vyombo vya habari.

Wanabunduki walishinda 2-1 dhidi ya Spurs katika mchezo wa Derby ya Kaskazini mwa London uliochezwa kwenye uwanja wa Emirates Jumatano usiku.

Spurs walianza kufunga kupitia nahodha wao Son Heung-Min kabla ya bao la kujifunga kutoka kwa Dominic Solanke na bao maridadi la winga LeandroTrossard kuwapa vijana wa Mikel Arteta uongozi.

Ushindi huo wa Jumatano usiku uliwaacha Arsenal wakiwa na alama 43 kwenye jedwali, na kuwasogeza karibu na vinara wa ligi Liverpool ambao wana alama 47 kwa sasa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved