Amad Dialo aliipa Manchester United ushindi baada ya kufunga mabao matatu chini ya dakika 12 za
mwisho za mchuano dhidi ya Southampton.
Ni zaidi ya miaka 91 tangu Manchester United kupoteza mechi zaidi
ya tatu mfululizo wakiwa katika uga wa old Trafford na Diallo winga mwenye
umri wa 22 alisaidia rekodi hiyo isivunjwe kwa kufunga hat trick chini ya dakika 12 kuanzia dakika wa 82 na kuipa
United ushindi wa 3-1.dhidi ya Southampton.
Southampton inayoshikilia nafasi ya mwisho katika jedwali ya
ligi ya Uingereza ilionekana kusumbua
vijana wa Amorim baada ya bao la kujifunga kutoka kwa mchezaji wa United Manuel Ugarte
katika dakika ya 43 kuwapa nafasi ya kuongoza 1-0 mpaka dakika ya 82.
Wakati kocha Erik Tenhag alitimuliwa 28 Octoba, 2024 Diallo alikuwa ameanza mechi
12 pekee tangia kujiunga na United kutoka katika klabu ya Atlanta mwaka wa 2021.
Winga huyo sasa hivi ameanza mechi 12 tangia Ten Hag
kuondoka ikiwa mechi ya kwanza alicheza chini ya mkufunzi Ruud Van Nistelrooy
na sasa anacheza chini ya Ruben Amorim.
Diallo amefunga mabao nane, likiwemo bao la dakika za lala
salama katika debi ya Manchester City, bao la kusawazisha dakika za lala salama
dhidi ya Liverpool na sasa amefunga hat-trick ya dakika 12 katika mechi ya
mwisho nyumbani dhidi ya klabu ya Southampton
ambayo ilikuwa ikitishia kushinda mchezo huo.
Diallo akihojiwa alisema kuwa katika mchezo wa kandanda kitu
muhimu sana ni kujiamini na kuaminia wachezaji wenzako.
‘’Katika Soka ni lazima na muhimu kuamini na tuliamini mpaka
mwisho,’’ alisema Diallo.
Diallo amekuwa tegemeo wa timu la Manchester United na ata
kuaminiwa na kocha wa United Amorim kucheza nafasi ya beki la kulia. Kufikia dakika
ya mwisho ya mchezo yao dhidi ya Southampton Diallo alikuwa akicheza kama
mshambuliaji.
‘’Niko tayari kucheza kila nafasi, niko tayari kucheza kama
beki wa pembeni, nambari 10, kila mahali meneja anapenda kuniweka niko tayari,’’ alisema Diallo akihojiwa baada ya mchezo.
Amorim alisema kwamba mambo mazuri yatatokea kwa raia huyo
wa Ivory Coast iwapo ataendelea kucheza na kufanya mazoezi vizuri.
‘’Mambo
mazuri yatatokea. Diallo yuko katika wakati mzuri na ana msimu mzuri sana ‘’ Alisema
Amorim.
United ilipanda hadi nafasi ya 12
kwenye ligi lakini kwa kiasi kikubwa mchezo yao ilikuwa chini dhidi ya Southampton licha ya ushindi huo wa dakika za mwisho.