Erling Haaland amesaini mkataba mpya wa miaka tisa na nusu katika Manchester City, uongozi wa timu umetangaza leo Ijumaa Januari 17.
Hili litamfanya yeye kusalia Etihad mjini Manchester mpaka mwaka wa 2034.
Manchester city ndio watetezi wa ligii kuu ya uingereza baada ya kuchukua ushindi mwezi Mei 2024.
Haaland mwenye umri wa miaka 24, mkataba wake ulikuwa unafaa kuisha mwezi Juni 2027, lakini sasa ameongeza mkataba huo na miaka zaidi ya sita, na sasa mkataba wake unamruhusu Haaland kubakia kwenye kikosi cha timu hiyo hadi mwaka 2034 iwapo hatauzwa au kupelekwa nje kwa mkopo.
Mwanasoka huyo mzaliwa wa taifa la Norway alijiunga na Manchester City kutokea klabu cha Borussia Dortmund mwaka 2022.
Kufikia sasa Haaland ameifungia City mabao 111 baada ya kucheza mechi 126.
“ Nina furaha ya ajabu kusaini mkataba mpya, sasa nina uwezo nikitizama mbele na kutumia muda wangu mwingi kuwa katika klabu hiki kikubwa,” alisema Erling Haaland.
“Manchester City ni klabu cha kipekee, kizuri na chenye watu wangwana wa kushikilia mkono. Ni eneo lenye makao mazuri na yanaweza kumpa kila mtu nafasi ya kufanya Mambo makubwa,” Haaland aliongeza.
Viongozi wa klabu cha Manchester pia wamesema , “ kila mmoja katika klabu ana furaha kwamba Erling Haaland amesaini mkatana mpya. Licha ya kwamba amesaini mkatab mrefu, inaonesha kujukumika kwetu kwake na upendo alio nao kwa klabu hiki. Amefanya mambo mazuri , makubwa na ya kushangaza na yawezajizungumzia.”
Kufikia sasa Haaland ameshinda Mataji saba akiwa na klabu ya manchester city.
(Mataji mawili ya ligii kuu uingereza, moja FA, ligi kuu ya mabingwa ulaya, UEFA, Fifa klabu mapambano ya dunia pamoja na kombe la maskio marefu).