logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rashford azungumza baada ya jarida kutishia kuchapisha picha yake akiwa na rapa muuaji

Rapa anayesemekana kuwa kwenye picha ya pamoja na Rashford ni muuaji aliyepatikana na hatia.

image
na Samuel Mainajournalist

Football17 January 2025 - 08:18

Muhtasari


  • Rashford ametoa taarifa kuhusu mpango wa jarida la habari za udaku wa kuchapisha picha yake akiwa na rapa mwenye utata.
  • "Nataka niweke wazi sijawahi kuona picha hii; Simfahamu mtu huyu na mimi si urafiki naye,” Rashford alisema.


Mshambulizi wa Manchester United, Marcus Rashford ametoa taarifa kuhusu mpango wa jarida la habari za udaku wa kuchapisha picha yake akiwa na rapa mwenye utata.

Katika taarifa yake Alhamisi jioni, mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 27 alifafanua kuwa hajawahi kuona picha hiyo iliyoripotiwa kupigwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Pia aliweka wazi kuwa hamfahamu mtu husika, na wala si rafiki naye.

"Nimepigiwa simu leo ​​na jarida la udaku likinijulisha kuwa wanapanga kuchapisha picha yangu na rapa inayeonekana kupigwa mwaka mmoja uliopita. Nataka niweke wazi sijawahi kuona picha hii; Simfahamu mtu huyu na mimi si urafiki naye,” Rashford alisema kwenye taarifa aliyoichapisha kwenye Instagram.

Aliongeza, "Kama wanasoka wengi wakati mtu akiniomba picha na mimi, sitakataa kamwe lakini ni wazi siwezi kufanya ukaguzi wa nyuma wa kila mtu anayeomba picha."

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye anahusishwa na uhamisho wa kuondoka Manchester United aliendelea kuvikosoa vyombo vya habari vinavyotishia kuposti picha hiyo na kuwataka kutumia jukwaa lao kwa mambo yenye manufaa.

"Tafadhali naweza kuhimiza magazeti ya udaku badala ya kuniangazia mimi, kutumia majukwaa yao kusaidia kutoa ufahamu juu ya mashirika mengi ya kutoa misaada na watu binafsi wanaofanya kazi kila siku nchini Uingereza kukabiliana na uhalifu wa visu ili kuzuia familia zaidi kupata hasara kubwa," alisema.

Taarifa kutoka Uingereza zinabainisha kuwa rapa huyo anayesemekana kuwa kwenye picha ya pamoja na Rashford ni muuaji aliyepatikana na hatia.

Kwa mujibu wa jarida la The Sun, Rashford kutaja jina la Mizen kunatoa dalili kubwa kuwa staa huyo wa United anazungumza kuhusu kupigwa picha na Jake Fahri, rapa anayejitambulisha kwa jina la kisanii TEN.

Fahri alihukumiwa kifungo kisichopungua miaka 14 jela mwaka wa 2009 kwa kumuua mvulana wa shule Mizen mwenye umri wa miaka 16 mnamo Mei 2008.

Hivi majuzi aliachiliwa kutoka gerezani na ameanza tena kufanya muziki.




RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved