Cristiano Ronaldo alipoulizwa lipi linafaa kufanywa katika timu ya Manchester United, alijibu akiserma kuwa angekuwa mmliki wa timu hio ya Uingereza angefanya Kinachostahili.
Ronaldo aliulizwa hili baada ya mashetani wekundu hao kupoteza mchuano wao dhidi ya Brighton & Hove Albion mnamo 19 January.
Kwa sasa timu hio inayocheza ligii kuu ya Uingereza inashikilia nafasi 13 kwenye ligii kuu ya EPL.
"Kama nikija kuwa mmiliki wa Manchester United, ningebadilisha kile kinachostahili." alisema Ronaldo.
Mchezaji huyo maarufu kutoka nchini Ureno amesema kuwa katika maisha yake ya baadaye ana imani kuwa atamiliki klabu kubwa ya kandanda.
" Kwa sasa mimi bado mdogo sana. nina mipango mingi na ndoto mbele yangu, lakini nakili maneno yangu, siku moja nitakuwa mmiliki wa klabu kubwa," aliongezea Ronaldo.
Cristiano Ronaldo ni mojawapo ya wachezaji ambao wamekuwa katika fani ya kandanda kwa muda mrefu zaidi, na amefaulu kuchezea timu tofauti tofauti na katika ligi tofauti. kwa sasa mchezaji huyo anaichezea timu ya Al-Nassr nchini Saudi Arabia.
Alijiunga na hiyo timu mwaka 2023, akitokea kilabu hiyo ya Manchester Untied. alivunja mkataba wake na klabu hiyo baada ya mkufunzi wa enzi hizo Erik Ten Hag kumuondoa katika kikosi cha kwanza cha timu. jambo ambalo lilimkasirisha na akamua kuondoka.
Kwa sasa CR7, ufupi wa jina lake pamoja na nambari ya jezi anayoivalia, ameshinda mataji 33. miongoni mwa mataji haya ni pamoja na mataji saba ya ligii alizoshiriki, mataji matano ya ligii kuu ya mabingwa ulaya na mataji mengine mengi kutoka nchi tofauti tofauti.
Ronaldo kufikia sasa amefunga magoli 917, na kutoa asisti 256, baada ya kucheza michezo 1,257 katika mpira wake wa utu uzima.
Magoli haya yanajumuisha yale aliyofunga katika vilabu alivyowahi kuvichezea pamoja na mabao aliyoyafunga kwa ajili ya taifa lake.
Kwa mchezaji huyo anaeyecheza kwenye nafasi kushambulia ndiye ameshilikilia rekodi ya dunia katika kufunga mabao mengi zaidi akifatiwa Lionel Messi mwajentina ambaye kwa sasa anachezea timu ya Inter Miami ilioko Marekani.