logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nahodha wa Chelsea Reece James aeleza kwa nini walipigwa na Man City

James alisikitishwa na mchezo wa timu yake baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Man City Jumamosi jioni.

image
na Samuel Mainajournalist

Football26 January 2025 - 10:43

Muhtasari


  • James alihisi kwamba The Blues walikosa kutumia nafasi zao vizuri baada ya kuchukua udhibiti wa pambano hilo mapema sana.
  •  James alibainisha kuwa City wamekuwa na muda mwingi pamoja tofauti na timu yao ambayo inaundwa na wachezaji wengi wapya.


Nahodha wa Chelsea Reece James alisikitishwa na mchezo wa timu hiyo baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Manchester City siku ya Jumamosi jioni.

Ingawa mshambulizi Noni Madueke aliiwezesha The Blues kupata mwanzo mzuri ndani ya dakika tatu, wenyeji walijibu kupitia Josko Gvardiol kabla ya kuchukua udhibiti baada ya kipindi cha mapumziko huku mabao ya Erling Haaland na Phil Foden yakifanikisha ushindi kwa vijana wa Pep Guardiola.

Beki huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 25 alihisi kwamba The Blues walikosa kutumia nafasi zao vizuri baada ya kuchukua udhibiti wa pambano hilo mapema sana.

"Inafadhaisha kutotoka na zaidi. Tulipata nafasi nyingine mapema baada ya kufunga na huenda mambo yalikuwa tofauti kidogo,” Reece alisema baada ya mechi hiyo ya kukatisha tamaa.

"Mabao ndiyo yanafanya wachezaji, kuunda timu, kushinda michezo na kushinda mataji na wakati mpira haupunguki kwako ni ngumu haswa unapocheza dhidi ya timu ngumu," aliongeza.

Nahodha huyo wa Chelsea hata hivyo alitambua maendeleo makubwa yaliyofanywa na timu hiyo msimu huu, akibainisha kuwa wanafanya kila wawezalo kupata matokeo bora.

Akiwalinganisha Chelsea na Man City, mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uingereza alibainisha kuwa mpinzani wao wa Jumamosi amekuwa na muda mwingi pamoja wa kufahamiana tofauti na timu yao ambayo inaundwa na wachezaji wengi wapya.

 "Ninapenda kufikiria tunafanya maendeleo ingawa matokeo hayaonyeshi hivyo kwa dakika. Ni vigumu kuona. Tunajitolea kwa kila kitu na tunatumai, matokeo yataanza kuonyesha juhudi zetu, "James alisema.

Aliongeza, "Ukiangalia, tumekuwa pamoja chini ya mwaka mmoja na wamekuwa pamoja kwa miaka saba labda - wamekuwa na muda mrefu zaidi wa kufanya kazi na meneja na timu. Bado tunajenga na tunatumai kuweka mambo sawa. Tunahitaji kuchukua mechi moja baada ya nyingine na kuona tuko wapi mwishoni mwa msimu.”

Baada ya kukiri jinsi matokeo yalivyokuwa ya kufadhaisha, Reece anaamini kwamba njia pekee ni kusonga mbele kwani The Blues wanatumai kurejea kutoka kwa kushindwa na wiki nzima ya maandalizi kuwa mbele ya West Ham wiki ijayo.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved