
Kocha mkuu wa Manchester United Ruben
Amorim mnamo Jumapili usiku alitania kwamba amezeeka kwa zaidi ya muongo mmoja
tangu achukue mikoba ya Erik ten Hag katika klabu hiyo.
Kocha huyo wa zamani wa Sporting Lisbon, ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa leo JumatatuJanuari 27, alisema anahisi kama anatimiza miaka 50 badala ya 40 baada ya miezi miwili ya kuwa Manchester United.
Mashetani wekundu walimpa Mreno huyo zawadi ya mapema kwa siku yake ya kuzaliwa kwa kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Fulham, shukrani kwa shuti lililopigwa na mlinzi Lisandro Martinez.
Ushindi huo ulikuwa wa nne pekee kwa Amorim kuonja mafanikio ya ligi tangu achukue mikoba kutoka kwa Erik ten Hag mnamo Novemba, huku mabingwa hao mara 20 wa ligi kuu wakiwa bado wanatatizika katikati mwa jedwali.
"Siyo 40… ninatimiza umri wa miaka 50. Baada ya miezi miwili nikiwa Manchester United ni miaka 50. Ni bahati nzuri kutimiza miaka 40 nikiwa hapa," Amorim aliambia BBC alipoulizwa kama ushindi wa Fulham ulikuwa zawadi nzuri ya siku ya kuzaliwa.
"Hisia hiyo ya kushinda na pointi tatu ni muhimu sana kwetu. Huwezi kuona maendeleo makubwa katika timu na huo ni ukweli. Lakini kushinda hutusaidia kuimarika,” aliongeza.
Amorim pia alikiri kukataa ombi la wachezaji kuchukua mapumziko Jumatatu akifichua kwamba watasherehekea siku yake ya kuzaliwa naye baada ya siku ya mazoezi.
"Waliomba siku ya mapumziko kesho,
sikuwapa, kwa hivyo tunafanya mazoezi kwa sababu ni siku yangu ya kuzaliwa na
zawadi yangu ni kufanya kazi na vijana ambao hawakucheza, itakuwa nzuri kwa
sababu tumeshinda. kula chakula cha jioni na watoto wangu," alisema.
Kilikuwa ni kipigo cha kwanza cha Fulham katika uwanja wa Craven Cottage tangu Novemba 23 na Amorim alikiri kwamba ana deni kubwa la shukrani kwa Toby Collyer, 21, ambaye aliweka kibali cha hali ya juu kuwanyima wenyeji bao la kusawazisha dakika za mwisho.
"Alifanya hivyo kwa mazoezi wakati mmoja. Toby aliokoa timu yetu leo," alisema Amorim.
Mshindi wa mechi, Lisandro Martinez pia alijawa na sifa kwa mchezaji mwenzake, akisifu tabia ya unyenyekevu ya Collyer.
"Nadhani nilikuwa na bahati, lakini
nimefurahishwa sana na jinsi tulivyoshinda mchezo. Haijalishi nani alifunga.
Pointi tatu muhimu zaidi, jinsi tunavyopigana, jinsi tunavyocheza,"
Martinez alisema kwenye TNT Sports. .
"Na jamaa huyu [Collyer]. Jamaa huyu ni mfano mzuri kwa kizazi kipya. Anafanya kazi kwa bidii na ni mnyenyekevu sana, anastahili yote," aliongeza.