Liverpool inayoshiriki kwenye ligi ya Uingereza imewaacha wachezaji 12 nje ya kikosi cha Champions League huku Arne Slot akielezea mabadiliko
Timu ya Liverpool imeshafaulu kupata nafasi kuingia katika mapambano ya kumi na sita bora katika ligi kuu ya mabingwa ulaya.
Liverpool ndio inayoshikilia nafasi ya kwanza na iwapo watashinda mchuano wao wa mwisho basi watakuwa wameshinda mechi zao zote katika hatua ya makundi.
Mkufunzi wa Liverpool aliamua kuwapumuzisha baadhi ya wachezaji wake ambao ni muhimu kuelekea mechi yao ya mwisho kwenye hatua ya makundi.
Wachezaji muhimu kuwaachwa nje ya kikosi cha Liverpool kumetajwa kama mpango wa kukwepa kumaliza nambari moja.
Hata hivyo iwapo liverpool watashinda mchuano wao wa leo ambao ndiyo wa mwisho bila shaka watamaliza juu ya jedwali.
Liverpool wanaongoza kwenye kinyanganyiro hicho wakiwa na alama 21, wakifuatwa kwa karibu na timu ya Barcelona ambao wako na alama 18.
Ushindi wa Barcelona na kupoteza kwa Liverpool huenda kukabadilisha kiongozi wa jedwali .
Kwa sasa Lverpool wana mabao 13, Barcelona nao wakiwa na mabao 15.
Mkufunzi wa Liverpool ameamua kuwaeka nje ya kikosi wachezaji muhimu kama vile Virgil van Djik na Mohamed Salah kwenye mapumziko baada ya ushindi wa mechi saba kati ya saba katika ligii hio.
Huenda mafanikio hayo yamewapa kiburi maanake tayari wana matokeo mazuri.
Mchuano wao wa mwisho wanaupiga leo dhidi ya PSV Eindhoven.
Slot alisema: "Imenichukua muda kuelewa muundo huu mpya lakini sasa nina uhakika wa asilimia 100 haijalishi kama utaishia kwanza au pili kwa sababu tumehakikishiwa kucheza timu ambayo ni ya 15, 16, 17 au 18, na kisha iko chini ya sare.
"Hatuwezi kuacha nafasi ya tatu. Haina athari kwenye meza ya ligi lakini tutajaribu kushinda. Mtu mwenye busara aliwahi kuniambia hajawahi kuona kitu chochote kizuri kutokana na kupoteza mchezo."
Alisson, Trent Alexander-Arnold, Ibrahima Konate, Ryan Gravenberch, Alexis Mac Allister, Dominik Szoboszlai, Luis Diaz, Joe Gomez, Diogo Jota na Curtis Jones wote waliachwa nyumbani pamoja na Salah na Van Dijk.
Kuachwa nje kunawapa mapumziko ya ziada kabla ya safari ngumu ya ugenini dhidi ya Bournemouth katika Ligi Kuu ya England Jumamosi wakati Wekundu hao wakitazamia kuendeleza uongozi wao wa pointi sita kileleni mwa jedwali.
Hawawezi kuanguka chini ya tatu huko Ulaya na alama moja katika PSV itawapa nafasi ya juu.