Kulingana na sheria mpya matokeo ya kila mechi yataamua kiwango cha jumla katika ligi mpya, na pointi tatu kwa ushindi na moja kwa sare bado inatumika.'
Timu nane za juu katika ligi zitafuzu moja kwa moja kwa raundi ya 16.
Kulingana na jedwali timu zifuatazo zimefuzu Katika hatua ya 16 bora: Liverpool, Barcelona, Arsenal, Inter Milan, Atletico Madrid, Bayer Leverkusen, Lille, Aston Villa.
Timu zinazomaliza katika nafasi ya 9 hadi 24 zitashindana katika hatua ya muanduano ili kutafuta njia yao ya kufikia hatua ya 16 bora ya mashindano.
Timu zinazomaliza nafasi ya 25 au chini zitaondolewa, bila kufikia Ligi ya Europa ya UEFA kama ilivyokua hapo awali.
Timu ambazo zimeondolewa ni: Dinamo Zagreb, Stuttgart, Shakhtar Donetsk, Bologna, Sparta Prague, Leipzig, Girona, Red Star Belgrade, Sturm Graz, Salzburg, Slovan Bratislava, Young Boys
Ili kuimarisha ushirikiano kati ya ligi za awamu za mtoano, na kutoa motisha zaidi ya michezo wakati wa awamu ya ligi, jozi za awamu ya mtoano pia zitaamuliwa kwa sehemu na viwango vya awamu ya ligi, na sare ambayo pia huamua na kuweka njia kwa timu kufikia fainali.
Katika awamu ya muondoano, timu zinazomaliza kati ya nafasi ya 9 na 16 zitapangwa katika awamu ya mtoano ya kucheza, ikimaanisha zitakutana na timu zinayoshikilia nafasi ya 17 hadi 24 - na, kimsingi, mguu wa kurudi nyumbani. [home & away]
Hizi ndizo timu zitakazoshiriki katika mechi za hatua ya mtoano: Atalanta, Borussia Dortmund, Real Madrid, Bayern Munich, AC Milan, PSV, Paris St-Germain, Benfica, Monaco, Brest, Feyenoord, Juventus, Celtic, Manchester City, Sporting, Club Brugge.
Klabu nane ambazo zitashinda katika awamu ya mtoano zitasonga mbele hadi raundi ya 16, ambapo kila moja itakabiliana na mmoja wa wamalizaji wa juu wa nane, ambao watapangwa katika raundi ya 16.
Michezo yote kabla ya fainali zitaendelea kuchezwa katikati ya wiki, kwa kutambua umuhimu wa kalenda ya ndani ya michezo kote Ulaya, wakati fainali itaendelea kuchezwa Jumamosi.
Kuanzia raundi ya 16 na kuendelea, ushindani utaendelea kufuata muundo wake uliokuepo wa raundi za mtoano ili kusababisha kufikia Finali kwenye ukumbi utakaochaguliwa na UEFA.
Baadhi ya timu ambazo zimeponea kwenye tundu la sindani ili kufaulu kusonga katika hatua ifuatayo ni pamoja Manchester City ilitoka nyuma na kuishinda Club Brugge na kuingia katika nafasi ya kucheza kwenye mechi za mchuano.
Aston Villa na Arsenal zilijiunga na Liverpool - ambao kwa muda mrefu walikuwa wamejikatia nafasi yao - katika hatua ya 16 bora kwani wao ndio wamemaliza juu ya jedwali.
Celtic, ambayo ilipoteza 4-2 dhidi ya Aston Villa, itakuwa katika mechi za mchujo pia hivyo timu zote tano za Uingereza zimesonga mbele katika awamu ya ligi.