Beki wa Manchester United Lisandro Martinez amechapisha ujumbe kwa wanasoka wenzake wa timu hiyo baada ya kufanyiwa upasuaji kutoka na jeraha lake alilopata kwenye mchuano dhidi ya Crystal Palace.
Muargentina huyo alipata jeraha katika mchuano ambao walishinda 2 - 0 katika uwanja wa Old Trafford. Duru zinaarifu kwamba huenda akakosa mechi zote zilizosaliasalia katika mwaka wa kalenda msimu huu.
'Ninahisi shukrani kubwa kwa kazi nzuri na msaada wa Man Utd, shirikisho la soka Argentina, familia yangu, marafiki, wachezaji wenzangu, na kila mtu aliyechukua muda kunitumia ujumbe wa kutia moyo. Upasuaji ulienda vizuri! Sasa ni wakati wa kutoa juhudo zangu, kwa moyo na roho, katika mchakato wa ukarabati," alieleza.
Martinez amekosa mechi zaidi ya 50 tangu ajiunge na United kutokana na jeraha, ingawa kurudi kwake hivi karibuni ni muhimu.
Martinez amekuwa mmoja wa wachezaji bora wa United tangu Ruben Amorim alipochukua mikoba ya Mashetani Wekundu mwezi Novemba, akifunga bao muhimu sana katika uwanja wa Anfield wakati United ilipochukua pointi moja dhidi ya wapinzani wao Liverpool mwanzoni mwa mwaka huu.
Akiandika kwenye Instagram, Martinez aliandika: "Leo, baada ya kupita siku kadhaa ngumu ambapo nilijiruhusu kuhisi na kukubali huzuni yangu, kutokuwa na msaada, kutokuwa na usalama, hofu, na usawa wa kihisia, ninaunganisha tena na kiini changu na maadili yangu, ambayo hunisaidia kuona vitu kutoka kwa mtazamo mzuri na mzuri zaidi,"
Beki huyo wa kati, aliyepewa jina la utani " The Butcher" kwa sababu ya mtindo wake wa kucheza, ni mmoja wa wachezaji kadhaa ambao kwa sasa wako katika chumba cha matibabu cha United - Amad Diallo, Manuel Ugarte, Kobbie Mainoo na Toby Collyer wote wamepata majeraha hivi karibuni
Kufikia sasa Martinez ameshinda mataji mawili na Manchester United yote yakiwa ya FA.
Lisandro Martínez mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Manchester United mnamo Julai 2022, akiungana tena na meneja wa zamani wa Ajax Erik ten Hag. Beki huyo wa Argentina alisajiliwa kwa ada ya karibu £57 milioni, na kuwa moja ya usajili wa juu zaidi wa dirisha la kwanza la uhamisho la meneja wa zamani wa Manchester United Erick Ten Hag.