logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Darwin Nunez atuma ujumbe maalum kwa mashabiki wa Liverpool kufuatia ukosoaji

Núñez ameonyesha msimamo thabiti dhidi ya ukosoaji unaoendelea kumwandama.

image
na Samuel Mainajournalist

Football20 February 2025 - 15:33

Muhtasari


  • Núñez amekuwa akilengwa na mashabiki na wachambuzi wa soka kutokana na ukame wa mabao na ufanisi wake mbele ya lango.
  • "Sikuwa bora zaidi wiki tatu zilizopita, wala hali si mbaya zaidi sasa. Nikidondoka, nitasimama tena," Nunez alisema.

Darwin Nunez

Mshambuliaji wa Liverpool, Darwin Núñez, ameonyesha msimamo thabiti dhidi ya ukosoaji unaoendelea kumwandama, akisisitiza kuwa hatakata tamaa na ataendelea kupambana kwa ajili ya timu yake hadi siku yake ya mwisho ndani ya kikosi cha The Reds.

Katika siku za hivi majuzi, Núñez amekuwa akilengwa na mashabiki na wachambuzi wa soka kutokana na ukame wa mabao na ufanisi wake mbele ya lango.

Licha ya kuonyesha bidii na kujituma uwanjani, mshambuliaji huyo wa Uruguay amekosa nafasi muhimu za kufunga mabao, jambo ambalo limewafanya baadhi ya mashabiki wa Liverpool kumkosoa vikali.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Núñez alijibu ukosoaji huo kwa maneno yenye msisitizo wa kujituma na uvumilivu:

"Sikuwa bora zaidi wiki tatu zilizopita, wala hali si mbaya zaidi sasa. Nikidondoka, nitasimama tena. Hamtaona nikikata tamaa. Nitatoa kila kitu hadi siku yangu ya mwisho hapa Liverpool. Uvumilivu!" aliandika Núñez.

Kauli hiyo imeonyesha uthabiti wa mchezaji huyo, ambaye tangu asajiliwe kutoka Benfica kwa dau kubwa la takriban pauni milioni 85 mwaka 2022, amekuwa akihitajika kuthibitisha thamani yake katika klabu hiyo. Licha ya kuonyesha kasi, nguvu, na ari ya kupambana, tatizo lake la umaliziaji limekuwa kikwazo kwa maendeleo yake.

Katika mechi kadhaa za msimu huu, Núñez ameonyesha uwezo wake kwa kufunga mabao muhimu, lakini ukosefu wa uthabiti umewafanya baadhi ya mashabiki kupoteza imani naye. Hata hivyo, wapo wanaomtetea, wakisema bado ana nafasi ya kujirekebisha na kuwa mshambuliaji hatari zaidi katika ligi.

Liverpool kwa sasa inashiriki mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza chini ya kocha Arne Slot, huku wakikabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa timu kama Arsenal na Manchester City.

Núñez anatarajiwa kushikilia nafasi muhimu katika kikosi hicho, hasa ikizingatiwa kuwa Liverpool inakabiliwa na mechi nyingi katika kipindi hichi.

Kwa kauli yake ya hivi karibuni, inaonekana Núñez anaelewa shinikizo analopitia, lakini hatakubali kushindwa kirahisi. Je, ataweza kuwanyamazisha wakosoaji wake kwa kiwango bora zaidi?

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved