Aliyekuwa meneja wa shirikisho la soka nchini Uhispania Luis Rubiales amepatikana na hatia ya kumbusu mchezaji Jenni Hermoso bila idhini yake na kuamriwa kulipa faini ya zaidi ya euro 10,000 (£8,275), Mahakama Kuu ya Uhispania imetoa uamuzi.
Wakati wachezaji wa Uhispania wakipokea medali zao baada ya kuwashinda England mjini Sydney na kushinda Kombe la Dunia 2023, Rubiales alimshika Hermoso kwa kichwa na kumbusu midomoni.
Tukio hilo lilisababisha maandamano na wito wa kujiuzulu kwa Rubiales.
Waendesha mashtaka walitaka hukumu ya kifungo kwa Rubiales, ambaye wiki iliyopita aliiambia mahakama kuwa alikuwa na "uhakika kabisa" Hermoso alikuwa amempa idhini kabla ya kumbusu.
Alielezea kuwa busu hilo lilikuwa kama "kitendo cha upendo", akiongeza kuwa kwa wakati huo ilikuwa "kitu cha hiari kabisa".
Katika ushahidi wake mapema mwezi huu, Hermoso alisisitiza kwamba hakumpa Rubiales ruhusa na kwamba tukio hilo "liliharibu mojawapo ya siku za furaha zaidi katika maisha yangu".
Rubiales alituhumiwa kwa unyanyasaji wa kingono na kujaribu kumlazimisha Hermoso kusema kuwa busu hilo lilikuwa la makubaliano, shtaka ambalo ameachiwa huru.
Tukio hilo lilishuhudiwa na mamilioni ya watazamaji wa televisheni na uwanja mzima baada ya timu ya wanawake ya Uhispania kushinda Kombe la Dunia la 2023.
kuibuka kwa kitendo hicho katika mchezo wa wanawake wa Uhispania, kulichochea zaidi ambapo wachezaji walitaka kupambana na vitendo vya ngono na kufikia usawa na wenzao wa kiume.
Rubiales alijiuzulu mwezi Septemba 2023 kufuatia wiki kadhaa za kupinga shinikizo za kuendelea kuhudumu, na baada ya FIFA kumsimamisha kazi, waendesha mashtaka wa Uhispania wakaanzisha uchunguzi.
Rubiales kabla ya kuwa meneja wa shirikisho la soka uhispania, alikuwa mchezaji wa kulipwa ambaye alicheza kama mlinzi, akionekana katika mechi 53 za La Liga kwa misimu mitatu.
Alikuwa rais wa Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF) na mmoja wa makamu wa rais wa ligi ya mabingwa UEFA.