Meneja wa timu ya Liverpol inayoshiriki ligii kuu Uingereza Arne Slot amezungumzia kikosi chake akionesha imani ya kumenyana na mahasimu wao Manchester City uwanjani Etihad siku ya juma pili.
Vinara hao wa ligii kuu uingereza wanakutana na City siku chache tu baada ya kutoka sare na vijana wa Aston villa.
Kwa upande wake amesema kwamba Man City ni timu kubwa kama vile Aston villa ambayo walicheza nayo, pia ameeleza kwamba watacheza kadri ya uwezo wao bila kuangalia matokeo ya Arsenal licha ya kwamba hao wapinzani wao wa karibu watacheza kabla yao.
"Nadhani swali kubwa la kuulizwa ni kutoka Man City kwa sababu tunakabiliana na timu imara tena, kama tulivyokabiliana na Villa. Arsenal inacheza mbele yetu lakini tunajua hiyo haifanyi mchezo kuwa rahisi au mgumu zaidi kuliko tulivyo nao dhidi ya City. Tunajua tuna mechi 12 za kucheza na Arsenal wana mechi 13 za kucheza," alieleza meneja huyo
Slot pia alisema kwamba wanatarajia upinzani mkubwa kutoka kwa Mancity, na wamejipanga kwa hilo. Pia amewakumbusha vijana wa Pep kwamba watakuwa wanakutana na timu ambayo haijapoteza kwa michuano 22. ambayo imepita.
"Ninachotarajia kutoka kwa City ni mapambano sababu Pep yupo: timu kubwa ya mpira wa miguu ambayo inaweza kucheza vizuri. Wako vizuri katika milki ya mpira. Lakini pia wanakabiliwa na timu imara ambayo haijapoteza mechi 22," meneja huyo aliwathahadharisha.
Slot ameeleza kwamba yuko na wachezaji wazuri ila bado anaendelea kuwajua vizuri kila siku, na ameelewa kwamba ni timu inayoweza kucheza mchezo mzuri kila bsaada ya siku tatu. Ameongeza akisisitiza kwamba yeye pamoja na mashabiki hawawezi kubali mchezo usio wa kujituma kwa asilimia kubwa.
"Daima tunajifunza katika kila mchezo lakini kwangu zaidi mambo ni sawa. Hivyo, wachezaji hawa wana uwezo wa kucheza kila baada siku tatu juu ya bora na uwezo wao.Lakini hatuwezi kukubali - sio mashabiki, wala mimi - kwamba hawatoi juhudi kubwa. Lakini hiyo ndiyo wanayofanya kila wakati na nadhani watafanya tena.- kwamba lolote lile tuna kukubali. Jambo zuri ni kwamba sisi hatupo nyuma ya mtu, sisi bado tuko nambari moja na ni jambo zuri. alifafanua zaidi meneja huyo wa vinara wa ligii.