Arne Slot anaamini Liverpool inahitaji kufanya vizuri zaidi ya mechi zote za msimu huu ili kufaulu kushinda Paris Saint-Germain { PSG] katika raundi ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
The Reds wanashikilia nafasi nzuri baada ya kunyakua ushindi katika mechi ya Jumanne usiku katika uwanja wa Anfield, kufuatia ushindi wa 1-0 walioupata.
Slot akizungumza na wanahabari alikiri kwamba mchuano kati ya Liverpool na PSG ni mojawapo ya mchezo muhimu sana kwake.
"Ndio, kwa sababu ni wa pili. Kwa sababu ni mchezo pili na mchezo ulio mbele huwa ni muhimu zaidi," asema Slot
Mkufuzi huyo alieleza kwamba PSG ni mojawapo ya timu ngumu ambazo amekutana nazo msimu huu na atafanya linalowezekana ili kufanikisha zaidi katika mchuano huo ujao katika mapambano ya pili Juma hili. Slot pia amelinganisha mchezo wa PSG na ule ambao walichuana na Arsenal pamoja na Manchester City.
"Ndio, nadhani hivyo kwa sababu hii ndio timu kamili zaidi ambayo tumekutana nayo hadi sasa. Ninachomaanisha kwa ukamilifu - na usawa, tumekabiliana na Arsenal na [Manchester] City na sio kwamba kuna kiwango kikubwa - lakini kiwango ambacho wamecheza pamoja na ubora walio nao... Wana ubora mwingi na meneja mzuri. Anairuhusu timu kucheza kwa namna ambayo si rahisi kucheza dhidi ya timu yake; Analeta ubora kutoka kwa kila mchezaji na huleta kiwango cha ajabu cha kazi katika timu. Kwa sababu hiyo, tunapaswa kuwa katika hali nzuri ya kesho. Lakini, kwa mfano, hatukuwa na umiliki wa mpira kabisa huko City ugenini lakini nyumbani tulikuwa na matokeo tofauti kabisa dhidi ya City kuliko tulivyokuwa tukicheza," alieleza kocha huyo.
Licha ya uwoga na wasiwasi Mkufunzi huyo wa Liverpool anaamini kwamba wana nafasi ya kuimarika na kupata ushindi utakaowawezesha kusonga mbele katika hatua ya robo fainali kwenye ligii ya mabingwa.
"Ni matumaini yetu kuwa tutamiliki mpira zaidi ya wiki iliyopita. Lakini tena, ukiwaona wakicheza, ni wakali sana wakati hawana mpira, jambo lililowafanya watengeneze nafasi chache tu. Lakini katika dakika ya 87 wakati mpira ulipokuwa na Alisson [Becker], walisonga mbele na wachezaji wengi, tulicheza kwa muda mrefu na walikuwa wazi, ambapo tuliweza kufunga bao letu. Nilipotazama mchezo baadaye, niliona nafasi nyinyi kwamba kama baadhi ya wachezaji wetu wangefanya vizuri basi hilo lingetupelekea kutengeneza nafasi. Pia najua kutokana na uzoefu wangu, kwa sababu kawaida timu yangu inafanya kile Paris Saint-Germain inafanya, kwamba kila meneja mwingine daima anasema, 'Tungeweza kufanya vizuri katika nyakati hizi za mpito," alisema.