logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sir Jim Ratcliffe aahidi kujenga uwanja wa kisasa zaidi duniani kwa Manchester United

Vilevile amefichua kwamba huenda akatafuta usaidizi wa serikali ya uingereza kumusaidia ili kufanikisha lengo lake kwa timu hiyo ya manchesater United.

image
na Japheth Nyongesa

Football11 March 2025 - 10:28

Muhtasari


  • Wakati huo ameongeza kwamba pesa sio changamoto lakini ataona cha kufanya na kuahidi kuzungumzia hilo jambo hivi karibuni..
  • "Fedha sio suala, nadhani suala si la  kifedha sana. Lakini maelezo ya kina ya kwamba tunataka kuzungumza juu ya hiyo siku zijazo. Itakuwa ya kuhusu kifedha, nadhani," alieleza.

Mmiliki wa asilimia kubwa ya hisa katika timu ya Manchester united inayoshiriki ligii kuu ya uingereza Sir Jim Ratcliffe amesema kwamba ana matumaini ya kujenga mojawapo ya viwanja vizuri zaidi duniani.

Mmiliki huyo akizungumza kwenye mahojiano na wanahabari pia amekiri kwamba kwa sasa timu hiyo ina changamoto za kifedha  lakini wako tayari kupigana na changamoto hiyo.

Vilevile amefichua kwamba huenda akatafuta usaidizi wa serikali ya uingereza kumusaidia ili kufanikisha lengo lake kwa timu hiyo ya manchesater United.

'Kama itaendelea, basi, nadhani, tunaunga mkono hilo kwa uwanja mpya. Kwa sababu ya miradi ya kuongeza mwanga unahitaji kiini, unahitaji moyo kwa mpango, vinginevyo ni mali ya makazi tu. Lakini nadhani kama tungejenga uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa zaidi duniani, ambao nadhani tutaufanya, basi hilo litavutia mashabiki bilioni ambao tumewapata duniani kote. Wote wanataka kwenda Manchester," alisema Ratcliffe.

Wakati huo ameongeza kwamba pesa sio changamoto lakini ataona cha kufanya na kuahidi kuzungumzia hilo jambo hivi karibuni. "Fedha sio suala, nadhani suala si la  kifedha sana. Lakini maelezo ya kina ya kwamba tunataka kuzungumza juu ya hiyo siku zijazo. Itakuwa ya kuhusu kifedha, nadhani," alieleza.

Mmiliki huyo wa Manchester united hata hivyo amekiri kuwepo na changamoto za kifedha hasa kwa matumizi ya timu, akitaja hilo kama linalochangiwa na matokea yasiyomazuri kwa timu ya manchester United.

"Ni suala rahisi. Kama unatumia zaidi ya wewe kupata hatimaye hiyo ni njia ya uharibifu. Kwa  misimu saba iliyopita, ikiwa utajumuisha msimu huu, klabu ingekuwa imepoteza pesa. misimu saba mfululizo. Nadhani hiyo ni jumla ya £330m, hivyo karibu theluthi moja ya fedha bilioni ambazo zimetoka nje ya klabu katika misimu minne au mitano iliyopita," alisema.

"Gharama za kuendesha klabu hiyo katika miaka saba iliyopita zimeongezeka kwa £100m. Gharama ya bili ya mshahara wa wachezaji katika miaka saba iliyopita au hivyo ni £ 100m. Ongezeko la mapato katika kipindi hicho ni £100m. Na kiasi hicho hakifanyi kazi. Kama unapoteza pesa kila mwaka, na wakati huo huo unaongeza gharama zako za kuendesha klabu, haifanyi kazi na inaishia katika shida. Na hapo ndipo klabu hii ingemaliza mwishoni mwa mwaka huu," alieleza mmiliki huyo akieleza kuhusu maamuzu ya timu hiyo ya mashetani wekungu kupunguza matumizi ya Fedha.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved