logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu hatima ya Manchester United na Tottenham kwenye ligi ya Europa

Manchester United walipata faida kwa kuishinda Real Sociedad katika hatua ya 16 bora kwenye mechi yao.

image
na Japheth Nyongesa

Football14 March 2025 - 08:47

Muhtasari


  • Michuano ya robo finali itafanyika tarehe 10 kwenye hatua ya kwanza na tarehe 17 kwenye hatua ya pili.
  • Fainali ya ligi ya Europa msimu huu imepangwa kufanyika Jumatano Mei 21 katika uwanja wa San Mames mjini Bilbao.

caption

Droo ya robo fainali ilifanyika wakati sawa na michuano ya mechi 16 bora  mwishoni mwa mwezi uliopita. Kwa sasa timu nane zilizoshindwa zimeondolewa. Timu ambazo zilitwaa ushindi zitakuwa zinaelekea katika mapambano ya robo finali.

Manchester United walipata faida kwa kuishinda Real Sociedad katika hatua ya 16 bora kwenye mechi yao. United watakuwa wanamenyana kwenye robo fainali dhidi ya Lyon, ambao waliifunga FCSB ya Romania kwa jumla ya mabao 7-1 katika mechi hizo mbili.

Hii ni mara ya kwanza kwa vilabu hivyo kukutana tangu mechi ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2008, na ni mara ya tatu tu kwa timu hizo kukutana katika hatua ya ushindani.

The Reds waliwafunga Real Sociedad 4-1 (5-2 kwa jumla) katika mechi ya raundi ya pili ya Alhamisi usiku na nahodha Bruno Fernandes alishuka wavuni  kwa hat-trick katika uwanja wa Old Trafford.

Tottenham Hotspur ilipindua upungufu wao wa jumla dhidi ya AZ katika mechi yao ya mwisho ya 16 na ni wazi kwamba  watakabiliana na washindi wa europa wa  2021/22 Eintracht Franfurt ili wafanikishe kusonga mbele.

Lazio itacheza mechi inayofuata dhidi ya Bodo/Glimt, wakati Athletic Club, inayotarajiwa kufika fainali katika ardhi ya nyumbani msimu huu ikicheza na Rangers, mabingwa wa  mwaka 2008 baada ya miamba wa Uskochi kuiondoa Fenerbahce ya Jose Mourinho kwa mikwaju ya penalti.

Rangers na Fenerbahce ziliingia katika mikwaju ya penalti, baada ya Waturuki kupindua pengo la magoli mawili katika mchezo wa Glasgow.

Michuano ya robo finali itafanyika tarehe 10 kwenye hatua ya kwanza na tarehe 17 kwenye hatua ya pili.

Bodo/Glimt Vs Lazio

Tottenham Vs Eintracht Frankfurt

Rangers Vs Athletic Club

Lyon Vs Manchester United

Fainali ya ligi ya Europa msimu huu imepangwa kufanyika Jumatano Mei 21 katika uwanja wa San Mames mjini Bilbao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved