Shirikisho la Soka nchini Kenya (FKF) limeamua kuwa AFC Leopards walipoteza mechi hiyo dhidi ya Mara Sugar FC kwa sababu mashabiki wao walisababisha mchezo kusimamishwa.
Mechi hiyo ya sehemu ya Kombe la MozzartBet, ilifanyika Jumamosi, Machi 8, 2025, kwenye Uwanja wa Jomo Kenyatta katika kaunti ya Kisumu. Mechi hiyo illichezwa mpaka dakika ya 80 wakati shida ilipozuka.
Kulingana na Kamati ya Ligi ya Mashindano ya FKF, mashabiki wa AFC Leopards walikimbilia uwanjani kupinga uamuzi wa mwamuzi.
Mwamuzi alikuwa amefuta penalti ambayo ilitolewa kwa mara ya kwanza kwa AFC Leopards, na mashabiki hawakufurahishwa na hilo.
Kamati hiyo ilifanya mkutano mnamo Machi 18, 2025, kuangalia kilichotokea. Walisoma ripoti kutoka kwa maafisa wa mechi na kusikiliza Mara Sugar FC na AFC Leopards. Baada ya kuangalia maoni ya pande zote, waliamua kuwa mashabiki wa AFC Leopard ndio wa kulaumiwa kwa kusimamisha mchezo.
Kwa sababu hio, kamati iliamua kwamba AFC Leopards walipoteza mechi hiyo. Hii inamaanisha kuwa Mara Sugar FC ilipewa ushindi na itasonga mbele kwa raundi inayofuata ya Kombe la MozzartBet. Uamuzi huo unafuata sheria za mashindano na sheria za mpira wa miguu hapa nchini Kenya.
Kamati hiyo pia iliionya AFC Leopards kuhusu tabia mbaya ya mashabiki wao. Waliiambia klabu hiyo kuchukua hatua za kukomesha ushabiki wa vurugu katika michezo yao katika siku zijazo.
Kamati ya Ligi ya Mashindano ya FKF imesema itatoa ripoti kamili inayoelezea uamuzi wao ndani ya siku 21. Taarifa hii itatoa maelezo zaidi kuhusu kwa nini walifanya uamuzi huo.
Habari hizi zinatokana na waraka rasmi wa FKF kuhusu mechi iliyotelekezwa, ikionyesha kwamba shirikisho hilo lina nia ya dhati ya kuhakikisha soka linakuwa salama na haki nchini Kenya.