Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alikuwa mmoja wa mashujaa wa Newcastle wakati walipomaliza kusubiri kwa miaka 70 kwa kombe la nyumbani siku ya Jumapili, na kuwalaza viongozi wa ligi ya Uingereza Liverpool 2-1 katika fainali ya kombe la Carabao katika uwanja wa Wembley.
Isak alifunga bao lake la 23 la msimu katika mashindano yote .19 ya miongoni akiyafunga kwenye ligi kuu ya uingereza.
Arsenal, Liverpool na Barcelona zimekuwa zikihusishwa na Isak, ambaye bila shaka huenda akazidisha mabao 25 aliyofunga msimu uliopita, huku wakiangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji bora wa kati mwenye uwezo wa kuwa kiungo muhimu wa timu yao kwa miaka ijayo.
Liverpool inadhaniwa kuwa katika mazungumzo na wawakilishi wa Isak kuhusu uwezekano wa kuhama, huku Arsenal ikiaminika kumtambua mchezaji huyo kama 'kipaumbele' chao.
Isak alijibu tena maswali kuhusu mustakabali wake ambapo yeye, bila kushangaza, aliongeza maradufu upendo wake kwa Newcastle huku akithibitisha kwamba umakini wake unabaki kwenye kile kinachotokea uwanjani badala ya nje ya uwanja.
"Hakuna mengi ya kusema, kwa kweli. Nimetoa maoni juu ya hali yangu na usalama wangu huko Newcastle mara kadhaa," Isak alisema. "Imeandikwa jinsi ninavyopenda jiji na klabu, jinsi ninavyohisi vizuri huko. Sifikirii juu ya siku zijazo. Nataka tu kucheza kwa Newcastle.
Mwanasoka huyo akizungumza amefichua kwamba lengo lake kubwa ni kucheza na Newcastle kwenye ligii kuu ya mabingwa ulaya.
"Sasa tumeshinda kombe, lakini tunataka kumaliza kwa nguvu na kufikia michezo ya Ligi ya Mabingwa. Hapo ndipo lengo langu liko. Hakuna sababu ya mimi kufikiria juu ya kitu kingine chochote (isipokuwa Newcastle). Ninajifurahisha vizuri sana huko Newcastle. Lengo pekee nililonalo ni kucheza," alieleza mchezaji huyo.
Ni Mohamed Salah na Erling Haaland pekee ambao wamefunga mabao mengi zaidi ya Ligi Kuu msimu huu kuliko Isak, ambaye amejiimarisha kama mmoja wa wachezaji bora zaidi wa soka duniani baada ya msimu wake wa kwanza huko St James' Park - ambao ulifuatia rekodi ya klabu ya uhamisho wa pauni milioni 63 msimu wa joto wa 2022 kuharibiwa na majeraha.