Harambee Stars watakuwa wanapambana katika mechi muhimu ya kufuzu kwenye Kombe la Dunia la FIFA 2026, Jumapili hii, tarehe 23 Machi 2025, saa kumi jioni.
Timu ya taifa ya Kenya itakabiliana na Gabon katika Uwanja wa Nyayo ulioko jijini Nairobi. Mechi hiyo ambayo ni muhimu kwa vijana wa kenya kwani iwapo watafaulu kutwaa ushind huenda ukawapa matumaini ya kufuzu katika kombe la dunia.
Kufikia sasa Kenya inashikilia nafasi ya nne katika Kundi F wakiwa na alama 6 baada ya kukamilika kwa mechi ya jana na kutoka sare ya 3-3 na Gambia.
Gabon ambayo itakuwa inapambana na Harambee Stars wanaongoza jedwali kwenye hicho kikundi kwa alama 12, Cote d’Ivoire, na Burundi wakifuata na alama saba kila mmoja.
Kwa mara ya kwanza tangu Novemba 2021, Kenya itapata fursa ya kucheza mechi nyumbani katika Uwanja wa Nyayo, baada ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kuridhishwa na maboresho yaliyofanywa kwenye uwanja huo.
Harambee Stars, chini ya kocha mkuu Benni McCarthy, wameonyesha nia thabiti ya kuleta mabadiliko katika timu.
Kenya ilipoteza mechi ya awali dhidi ya Gabon kwa mabao 2-1 ugenini, ila wana imani kwamba wana nafasi ya kupata matokeo mazuri nyumbani.
Harambee Stars kutoka nyuma mabao mawili na kutoka sare na Gambia kwenye uwanja wa Alassane Ouattara mjini Abidjan Alhamisi usiku. ulionesha maazi uwezo wa timu hiyo kwa kutokata tamaa.
Vijana wa Benni McCarthy waliendelea kujituma mpaka dakika za mwisho wakati Kiungo wa kati anayecheza Australia Wilson Lenkupae alipofunga katika dakika za mwisho (dakika ya 96) na kusawazisha mechi kwa 3-3.
Matokeo hayo yanamaanisha Stars waliondoka kwa Gambia wakiwa na moja na kumpa McCarthy sare yake ya kwanza kama Kocha mkuu wa Stars.