Mwanasoka huyo alieleza kwamba kilichomchochea zaidi ni kutokana na sababu kwamba familia yake kubwa iko hapa kenya na amekuwa na uhusiano wa karibu na taifa la Kenya.
“Ilikuwa wazo zuri kichwani mwangu, na nilihisi huu ulikuwa wakati mwafaka kwangu. Nimekuwa na uhusiano wa karibu na Kenya kila wakati. Baba yangu yupo hapa, mjomba wangu yupo hapa, familia yangu ipo hapa, kwa hivyo daima nimekuwa na mshikamano na nchi hii," alieleza Lenkupae.
Willson Lenkupae alizaliwa Australia akiwa na asili ya wakenya kutoka kabila la Samburu, alichagua kuwakilisha Kenya badala ya Australia.
Alipokea mwito wake wa kwanza wa kimataifa katika timu ya taifa ya Kenya mnamo Machi 2025 kwa mechi zao za kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 dhidi ya Gambia na Gabon. Mnamo tarehe 20 Machi, alifunga bao lake la kwanza katika sare ya mabao 3 dhidi ya Gambia.
William Lenkupae aliyezaliwa 23 Disemba 2001 ni mchezaji wa soka wa Kenya ambaye anacheza kama kiungo wa katika klabu ya Central Coast Mariners ya Australia na timu ya taifa ya Kenya.