Shirikisho la soka nchini Kenya FKF, likitoa uamuzi huo limerejelea video ambayo imesambazwa mitandao ikimuhusisha mwanasoka huyo na madai ya ubadhirifu wa michezo ambayo ni hatia kubwa kwa wanasoka wote duniani.
FKF kwenye barua iliofikia sitesheni ya Radio Jambo imetoa tangazo kwamba mchezaji huyo atakua inje ya soka la kulipwa kwa siku 90 huku uchunguzi ukiendela kufanyika. Usimamizi wa shirika hilo limeeleza kwamba maamuzi hayo yako ni sahihi kulingana na sheria za michezo nchini.
"Shirikisho la soka nchini Kenya [FKF] limempa likizo ya muda mlinda lango Patrick Matasi kutoshiriki kwa shughuli zote ambazo zipo chini ya FKF kwa muda wa siku 90. Maamuzi haya yanatokana na video ambayo inasambaa inayoonesha uwezekano wa kuiuka kwa sheria za michezo," barua ilisomeka.
"Maamuzi haya yamefanyika kulingana na sheria kifungu VII [2] ya FKF ya ukiukaji wa sheria za michezo ya mwaka 2016. Hili limefikishwa kwa timu ya soka ya Kakamega Homeboys na mchezaji husika," barua iliendelea.
Wakati huo huo shirikisho la FKF pia limesema kwamba liotahusisha mamlaka tofauti tofauti ilikiwa ni pamoja mashirikisho mengine ya soka kama vile FIFA na CAF ili kuhakikisha uchunguzi wa wazi kwa wahusika wote.
"FKF itashirikiana na FIFA, CAF na mamlaka mengine husika. Uchunguzi umeanzishwa kuhusu hilo swala. Shirikisho litasailia wazi kushikilia viwango vya soka nchinina kuhakikisha kuna uwazi wa kutosha kwa sehemu zote husika,' barua hiyo ilisomeka zaidi.