logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Olunga kumenyana na Salah, Lookman, Mane kwa tuzo ya mchezaji bora Afrika 2025

Michael Olunga ameteuliwa kuwa miongoni mwa wawaniaji wa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika.

image
na Japheth Nyongesa

Football02 April 2025 - 08:31

Muhtasari


  • Olunga mwenye umri wa miaka 31 atawania tuzo hio ya mchezaji bora wa kiume akimenyana na majina tajika kwenye ulingo wa soka la Afrika.
  • Winga wa Manchester United Amad Diallo (Ivory Coast) pia ameingia kwenye orodha hiyo, pamoja na Franck Kessié wa taifa hilo hilo.
Michael Olunga
Nahodha wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, Michael Olunga ameteuliwa kuwa miongoni mwa wawaniaji wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika.

Olunga mwenye umri wa miaka 31 atawania tuzo hiyo ya mchezaji bora wa kiume akimenyana na majina tajika kwenye ulingo wa soka la Afrika.

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Kenya na Al Duhail ya Qatar  atakuwa akiwania tuzo hii inayotamaniwa na wengi pamoja na mchezaji bora wa Afrika wa 2024, Ademola Lookman wa Nigeria, na mfungaji bora wa muda wote na nahodha wa Senegal Sadio Mané.

Mchezaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah ambaye ni mshindi wa tuzo hiyo mara mbili pia ameingia kwenye orodha hiyo.  Stéphane Aziz wa Burkina Faso anayechezea ligii ya Tanzania kwenye timu ya Yanga ni miongoni mwa walioorodheshwa. 

 Orodha hio iliyojaa nyota ya wachezaji bora bado inawajumuisha wachezaji maarufu  kama  Kalidou Koulibaly wa Al Hilal SFC ya ligii ya Saudi na Senegal, mlinda lango maarufu wa Manchester United na timu ya taifa ya Cameroon Andre Onana.

Wateule wengine mashuhuri ni pamoja na Achraf Hakimi wa Morocco, mchezaji wa zamani wa Manchester United Eric Bailly (Ivory Coast), kiungo wa kati wa Arsenal na mchezaji wa kimataifa wa Ghana Thomas Partey, pamoja na mwenzake Mohammed Kudus wa West Ham United.

Winga wa Manchester United Amad Diallo (Ivory Coast) pia ameingia kwenye orodha hiyo, pamoja na Franck Kessié wa taifa hilo hilo

Osimhen alishinda tuzo hiyo mnamo 2023 na anaweza kurejea kwa nyingine mnamo 2025 ikiwa ataendelea na kasi yake. Kwa sasa yuko kwa mkopo huko Galatasaray kutoka Napoli. Kama ilivyobainishwa mchango wake wa mabao umewafanya mabingwa hao wa Uturuki kufuata uhamisho wa kudumu.

Nicolus Jackson alikosolewa vikali wakati wa msimu wake wa kwanza huko Chelsea, Licha ya kuwa inje kwa muda kutokana na majeraha msimu huu ana mabao tisa na asisit 2.

sherehe za huu mwaka zitafanyika nchini Morocco.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved