logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilikuwa refa wa EPL lakini sasa najifunza kutembea tena - Rennie

Alikuwa mwamuzi wa kwanza mweusi wa Ligi Kuu ya Uingereza.

image
na Japheth Nyongesa

Football03 April 2025 - 15:20

Muhtasari


  • Baada ya kukaa kwa miezi mitano hospitalini, mzee huyo mwenye umri wa miaka 65 amezungumza .
  • "Imebidi nijifunze kutembea tena, ninarekebisha miguu yangu." alisema.
caption

Uria Rennie alifahamika na mamilioni ya mashabiki wa soka baada ya kuwa muamuzi wa kwanza mweusi wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Mara baada ya kutajwa kuwa afisa wa mechi "aliye sawa zaidi" katika soka la kimataifa na mtaalam wa sanaa ya karate, sasa anajifunza kutembea tena baada ya hali adimu ya kiafya iliyomfanya kupooza kuanzia kiunoni kwenda chini.

Baada ya kukaa kwa miezi mitano hospitalini, mzee huyo mwenye umri wa miaka 65 amezungumza na BBC News kuhusu ukarabati, ari yake ya kukabiliana na hali yake na jukumu jipya kabisa.

Rennie, ambaye alisimamia zaidi ya mechi 300 za ligi kuu kati ya 1997 na 2008, alikuwa katika safari ya kusherehekea siku ya kuzaliwa Uturuki mwaka jana alipokumbwa na maumivu ya ghafla kwenye mgongo wake.

"Nilidhani nilikuwa nimelala tu kwenye chumba cha kupumzika cha jua, nilitarajia kwenda upanda mwavuli angani lakini kwasababu ya maumivu ya mgongo sikuweza kwenda," anasema.

"Mwisho wa likizo sikuweza kulala , nilikaa macho kutokana na maumivu, na nilipofika nyumbani nilitembea kwa shida."

Rennie aliweka historia mwaka wa 1997 aliposimamia mechi kati ya Derby County na Wimbledon, na kuwa mwamuzi wa kwanza mweusi wa daraja la juu.

Mwanaume huyu ambaye ni mrefu kwa kimo na mtaalam wa ndondi za mateke na aikido, wachezaji waliokuwa wakipinga waligundua kwa haraka kwamba alikuwa amejiweka sawa wakati wa makabiliano

Akiwa mwamuzi huko Sheffield tangu 1996, amefanya kampeni katika masuala kama vile kuboresha usawa na ushirikishwaji katika michezo, kusaidia afya ya akili na kukabiliana na kunyimwa.

Rennie alikuwa kwenye harakati za kuanza kazi mpya kama Chansela wa Chuo Kikuu cha Sheffield Hallam alipolazwa katika Hospitali Kuu ya Kaskazini mnamo Oktoba.

"Nililala kwa mwezi mmoja chali na miezi minne mingine huku nikiwa nimekaa kitandani," alisema.

"Waliniweka hospitalini hadi Februari, walikuta kinundu kikinisukuma kwenye uti wa mgongo na ilikuwa ni hali ya nadra ya mishipa ya fahamu hivyo si kitu ambacho wanaweza kukifanyia upasuaji.

"Imebidi nijifunze kutembea tena, ninarekebisha miguu yangu."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved