Shirika la Kenya Power limetangaza kuwa maeneo mbalimbali katika kaunti tano yatakumbwa na kukatika kwa umeme Jumatano, kutokana na shughuli za matengenezo ya mtandao wa usambazaji.
Kaunti zitakazoathirika ni Nairobi, Kajiado, Elgeyo Marakwet, Kakamega na Nyeri, huku kampuni hiyo ikiwataka wateja kupanga shughuli zao mapema.
Katika Kaunti ya Nairobi, wakazi wa mtaa wa Ngumba pamoja na maeneo jirani hawatakuwa na umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.
Kwa upande wa Kaunti ya Kajiado, umeme utakatika kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika eneo la Matasia, ikiwemo Saina, Bluesky, Oloosuyian, Oloyankalani, Saab Royal, Suguna Feeds, Hospitali ya Rufaa ya Kajiado, Masai Polytechnic, Moipei, Sambel, Tata Chemicals, Esokota, Uwanja wa Ndege wa Saina, Mji wa Kajiado, pamoja na maeneo yanayozunguka. Serikali ya Kaunti ya Kajiado pia imo miongoni mwa taasisi zitakazoathirika.
Katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet, maeneo ya Chepsirei na Kapkayo yatakumbwa na kukatika kwa umeme kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo yatakayoathirika ni pamoja na Chuo cha Ufundi cha Chepsirei (TTI), Chepsirei NYS, Soko la Kapkayo, Soko la Kocholwo, Teber, Setano, Enego, na wateja walioko karibu.
Kwa wakazi wa Kaunti ya Kakamega, hasa eneo la Matungu, kukatika kwa umeme kutaanza saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo husika ni pamoja na Shule ya Msingi ya Kholera, Kijiji cha Kholera, Soko la Matungu, Soko la Harambee, Mayoni, Panyako, Bulimbo, Koyonzo, na vitongoji vinavyopakana.
Katika Kaunti ya Nyeri, maeneo ya Rititi na Gatunganga hayatakuwa na umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo yaliyoathiriwa ni Soko la Rititi, Cheru, Kianjogu, Kiwanda cha Kianjogu, Soko la Thaithi, Chemchemi ya Mahiga, Gatiko, Kinguku, Soko la Ngaini, Rathithi, Kiwanda cha Kahira-Ini, Gatunai, Soko la Gatunganga, Kijiji cha Mukanyaritho, Maganjo, Shule ya Upili ya Maganjo, Soko la Chieni Mikundi, Shule ya Upili ya Hiriga, Manorero, pamoja na booster za Safaricom na Airtel.
Vituo vingine vitakavyoathiriwa na
kukatika kwa umeme ni pamoja na Chriss
Pole Yard, Hoteli ya Lusoi, Pampu ya Maji ya Thung’ari, na Everest.
Kenya Power imeomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza na kuwasihi wateja kupanga shughuli zao kwa mujibu wa ratiba hiyo