Michael Olunga aachwa nje kikosi cha Harambee stars

Timu hiyo inatarajiwa kuanza maandalizi jijini Nairobi kuanzia Jumanne.

Muhtasari

•Michael Olunga hajapokea mwito katika kikosi cha Harambee Stars kwa mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia 2026 dhidi ya Burundi na Ivory Coast.

•Kenya inaratibiwa kuchuana na Burundi kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia 2024.

Michael Olunga. Picha;Facebook
Michael Olunga. Picha;Facebook

Nahodha wa Harambee Stars Michael Olunga hajajumuishwa katika kikosi cha muda cha Engin Firat kwa ajili ya michuano ijayo ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026 dhidi ya Burundi na Ivory Coast.

Tangazo la kikosi lilikuja Jumatatu kutoka kwa kocha mkuu Engin Firat.

Olunga amekuwa nguzo kwenye mashindano yaliyopita. Kutokuwepo kwake kunazua maswali kuhusu mipango ya timu dhidi ya wapinzani wakubwa kama vile Ivory Coast, ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Mataifa ya Afrika.

Orodha ya kocha huyo inajumuisha wachezaji 25, wakiwa na mchanganyiko wa wachezaji wenye uzoefu wa kimataifa na wenye vipaji chipukizi.

Hasa, Brian Okoth kutoka Kenya Police ameitwa kwa mara ya kwanza, akitambuliwa kwa uchezaji wake bora katika ligi ya humu nchini. Wengine walioingia kwenye orodha hiyo ni Austine Odhiambo kutoka Gor Mahia, anayeongoza Ligi Kuu ya FKF kwa kutoa pasi za mabao, na Adam Wilson kutoka Bradford City nchini Uingereza.

Miongoni mwa waliorejea ni Duke Abuya na Elvis Rupia, ambao walikosa mchuano wa mwisho wa mataifa manne lakini wameonyesha kiwango kizuri katika vilabu vyao. Kujumuishwa kwa Tobias Knost kutoka SV Verl ya Ujerumani na Bruce Kamau kutoka Perth Glory ya Australia kunaongeza uzoefu wa kimataifa kwenye kikosi.

Timu hiyo inatarajiwa kuanza maandalizi jijini Nairobi kuanzia Jumanne, Mei 21, 2024, huku mechi yao ya kwanza dhidi ya Burundi ikipangwa Juni 7, ikifuatiwa na mtanange na Ivory Coast mnamo Juni 11. Mechi zote mbili zitafanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa Bingu mjini Lilongwe, Malawi, kutokana na kutokuwepo kwa viwanja vinavyofaa nchini Kenya.

                     Kikosi cha Harambee Stars

Makipa

Patrick Matasi (Kenya Police], Byrne Odhiambo (Bandari), Boniphas Munyasa (Muranga Seal), Ian Otieno (Zesco, Zambia)

Mabeki:

Johnstone Omurwa (Estrela, Ureno), Alphonse Omija (Dhofar-Oman), Amos Nondi (Ararat, Armenia), Brian Okoth (Kenya Police), Abud Omar (Kenya Police), Tobias Knost (SV Verl, Germany)

Viungo wa Kati:

John Ochieng (Zanaco, Zambia), Eric Johanna (UTA, Romania), Adam Wilson (Bradford City, Uingereza), Anthony Akumu , Kenneth Muguna (Kenya Police), Kaycie Odhiambo (AFC Leopards), Chrispine Erambo ( Tusker), Rooney Onyango (Gor Mahia), Ayub Timbe (Sabail, Azeberijan), Duke Abuya (IHEFU, Tanzania), Bruce Kamau (Perth Glory, Australia)

Washambuliaji:

John Avire (El Sekka El Hadid SC, Misri), Austine Odhiambo (Gor Mahia), Benson Omala (Gor Mahia), Elvis Rupia (IHEFU, Tanzania)