UEFA yachunguza baada ya kelele za kufanya mapenzi kutatiza matangazo ya droo ya Euro 2024

Mburudishaji Daniel Jarvis alikuwa nyuma ya kipindi hicho na pia amekiri kuhusika na tukio hilo la aibu.

Muhtasari

•Uefa imeanzisha uchunguzi baada ya kelele za ngono kusambazwa wakati wa matangazo ya droo ya Euro 2024 siku ya Jumamosi.

•Jarvis aliwaambia watazamaji: "Sikiliza ilikuwa sisi, ilikuwa sisi. Tuliiingiza mle, tukaweka simu mle, tukaipigia, kelele za ngono kwenye droo ya Euro 2024."

wakati wa matangazo ya droo ya Euro 2024 mnamo Disemba 2, 2023.
Naibu katibu mkuu wa Uefa, Giorgio Marchetti wakati wa matangazo ya droo ya Euro 2024 mnamo Disemba 2, 2023.

Uefa imeanzisha uchunguzi wa kina baada ya kelele za ngono kusambazwa wakati wa matangazo ya moja kwa moja ya droo ya Euro 2024 mnamo Jumamosi, Desemba 2.

Wakati wa droo hiyo ya moja kwa moja ambayo ilipeperushwa na BBC kutoka Hamburg, Ujerumani, kelele chafu zilisikika wakati Uswizi ikipangwa katola Kundi A pamoja na Scotland, Hungary na wenyeji Ujerumani. Kelele za sauti ya mwanamke wakati wa mapenzi zilisikika mara kadhaa nyuma ya matangazo ya moja kwa moja wakati wa droo ya mashindano hayo ya bara Uropa ambayo ilikuwa ikifanyika kwenye ukumbi wa Elbphilharmonie.

Wakati wa kelele hizo, kulikuwa na mabadiliko ya sura na kejeli kutoka kwa vigogo wa soka waliokuwa kwenye umati wa watu, huku mastaa wa zamani wa Manchester City, David Silva na mwanasoka wa Denmark, Brian Laudrup wakijaribu kudumisha utulivu wao huku wakiendelea kumakinika  licha ya usumbufu usio wa kawaida.

"Kuna kelele hapa... hiyo imekoma," naibu katibu mkuu wa Uefa, Giorgio Marchetti alisema baada ya kukamilika kwa droo ya Kundi A.

"Hakuna kelele tena..." aliongeza, kabla ya kelele hizo kubwa kuanza tena pale Italia ilipotajwa kama timu ya mwisho katika Kundi B pamoja na Uhispania, Albania na Croatia.

Mwimbaji na mcheza mizaha wa YouTube Daniel Jarvis - AKA Jarvo69 - alikuwa nyuma ya kipindi hicho na pia amekiri kuhusika na tukio hilo la aibu.

Jarvis alijitangaza moja kwa moja kwenye mtandao wa X, ambaoo zamani ulikuwa Twitter, akipiga simu ya rununu mara kwa mara ili kuzua kelele wakati droo ya Euro, ambayo ilipeperushwa na runinga ya BBC kutoka jijini Hamburg, Ujerumani.

Jarvis aliwaambia watazamaji: "Sikiliza ilikuwa sisi, ilikuwa sisi. Tuliiingiza mle, tukaweka simu mle, tukaipigia, kelele za ngono kwenye droo ya Euro 2024."

Hii sio kelele ya kwanza ya ngono kwenye kipindi cha moja kwa moja wa BBC katika miaka ya hivi karibuni, tukio kama hilo lilitokea Januari wakati wa mazungumzo ya kabla ya mechi ya Kombe la FA kati ya Liverpool na Wolves kupeperushwa.