Beki mahiri wa klabu ya Arsenal William André Gabriel Saliba kwa sasa yuko katika nchi yake ya asili, Cameroon.
Katika kipindi cha siku chache zilizopita, mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 22 ameonekana katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi akifurahia muda na baadhi ya wanafamilia na mashabiki wake.
Pia alikutana na nyota wa zamani wa soka wa nchi hiyo Samuel Eto’o ambaye alishiriki muda naye na hata kutazama mechi ya soka naye katika moja ya viwanja nchini Cameroon. Eto'o , 42, kwa sasa ndiye rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon kuanzia tarehe Desemba 2021 kufuatia kustaafu mwaka 2019.
Saliba tayari ametangazwa kutoweza kuichezea klabu yake ya Arsenal katika mechi zilizosalia za msimu wa 2022/23 EPL kwani bado anauguza jeraha la mgongo. Hajaweza kuwachezea wanabunduki tangu Machi alipojeruhiwa wakati wa mchuano wa Ligi ya Europa dhidi ya klabu ya Sporting Lisbon.
Mchezaji huyo mahiri wa timu ya taifa ya Ufaransa aliamua kutumia likizo yake ya jeraha kuwatembelea wanafamilia wake nchini Cameroon. Marehemu mama yake anaamikia kutoka nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilhali baba yake, Brian Robertson alitoka nchi ya Lebanon, barani Asia.
Kwa bahati mbaya, Saliba aliwapoteza wazazi wake wote wawili miaka michache iliyopita, babake akitangulia.