Shujaa 7s wabanduliwa nje ya michuano ya Olimpiki inayoendelea jijini Tokyo

Matokeo hafifu ya mechi dhidi ya Ireland ambayo ilichezwa mapema asubuhi ya kuamkia Jumanne yalikatiza ndoto za Shujaa 7s.

Muhtasari

•Hii ni baada ya timu hiyo kupoteza mechi zake zote  tatu kwenye kundi la C

• Ireland ilishinda 12-7 na kubandua Shujaa kwenye Olimpiki.

Shujaa 7s
Shujaa 7s
Image: HISANI

Timu ya taifa ya raga ya wachezaji 7 kila upande, Shujaa 7s imebanduliwa nje ya michuano ya olimpiki inayoendelea jijini Tokyo Japan.

Hii ni baada ya timu hiyo kupoteza mechi zake zote  tatu kwenye kundi la C . 

Shujaa walipoteza mechi ya kwanza dhidi ya Marekani  baada ya kuzoa pointi 14 na Marekani kupata 19 siku ya Jumatatu.

Kwenye mechi ya pili Shujaa waliangamizwa na Blitzboks ya Afrika Kusini  5-14 na matumaini yote ya timu hiyo kuendelea na safari yake ya Olimpiki yakawa kwenye mechi yake ya mwisho kwenye kundi C dhidi ya Ireland.

Matokeo hafifu ya mechi dhidi ya Ireland ambayo ilichezwa mapema asubuhi ya kuamkia Jumanne yalikatiza ndoto za Shujaa 7s. Ireland ilishinda 12-7 na kuwabandua nje Shujaa kwenye Olimpiki.