Hongera! Shujaa 7s, Kenya Lionesses waibuka bingwa katika mashindano ya Safari 7s

Muhtasari

•Shujaa 7s walipiga Ujerumani 12-5 katika fainali ya kukata na shoka ambayo ilifanyika siku ya Jumapili na kuwezesha Kenya kuhifadhi taji hilo ambalo lilishindwa na Kenya Morans mwaka wa 2019.

•Lionesses walipata ushindi mkubwa wa 26-0 dhidi ya Uganda cranes katika fainali  ya mashindano hayo.

Image: HISANI

Timu ya taifa ya rafa Shujaa 7s iliweza kushinda mashindano ya Safari 7s 2021 ambayo yakifanyika ugani Nyayo wikendi iliyotamatika.

Shujaa 7s walipiga Ujerumani 12-5 katika fainali ya kukata na shoka ambayo ilifanyika siku ya Jumapili na kuwezesha Kenya kuhifadhi taji hilo ambalo lilishindwa na Kenya Morans mwaka wa 2019.

Alvin 'Buffa' Otieno na Johhnstone Olindi walifungia Shujaa 7s huku Jack Hunt akifungia Ujerumani.

Collins Shikoli alionyeshwa kadi nyekundu kwa kucheza katika kipindi cha pili ila jambo hilo halikukatiza matumaini ya Shujaa ya kupata ushindi. Ujerumani pia walipunguzwa hadi wachezaji sita baada ya mmoja wao kuonyeshwa kadi nyekundu muda mfupi baadae.

Timu ya wanawake ya Kenya Lionesses pia  ilibuka bingwa baada ya kushinda mechi zake zote.

Lionesses walipata ushindi mkubwa wa 26-0 dhidi ya Uganda cranes katika fainali  ya mashindano hayo.