- Huku seneta wa Nairobi Sifuna akizungumzia suala hilo, kupitia kwenye ukurasa wake twitter ameapa kuwapa wachezaji hao elfu 100
Wachezaji wa raga wa Kenya ambao wanadai mshahara lazima watafute pesa za kuchezea nchi yao.
Kikosi cha raga ya Kenya kwa sasa kinaangazia kukusanya pesa ili kusafiri na kuwakilisha taifa katika safu ya Dubai 7s mnamo Desemba 2-3 na HSBC Cape Town Sevens, itakayoanza Desemba 9, 2022.
Kulingana na mchezaji Willy Ambaka, timu haijalipwa kwa miezi mitatu.
"Kama baadhi yenu mnavyofahamu, huu ni mwezi wa tatu sasa tunapita bila malipo. Ingawa tumekuwa tukifanya kazi kwa bidii ili kuwapa matokeo mnayoyataka uwanjani, maisha yetu na ya wapendwa wetu yamewekwa chini ya dhiki kubwa.
Huku seneta wa Nairobi Sifuna akizungumzia suala hilo, kupitia kwenye ukurasa wake twitter ameapa kuwapa wachezaji hao elfu 100.
Pia amemtaka waziri wa michezi Namwamba kufanya jambo kwa ajili ya maisha ya wachezaji hao.
"Nitakuanza na 100k @Wilyambaka . Tunajivunia kazi unayofanya licha ya magumu. Pia nimezungumzia suala hili katika Seneti na wiki jana suala hilo lilichukuliwa na kamati husika. Msaada uko njiani, subiri. @AbabuNamwamba hizi ni nini?"
"Kwa sababu ya hali yetu hatari, sasa tunakugeukia wewe, jumuiya yetu ya kimataifa, kwa usaidizi wa kutafuta fedha. Tunahitaji msaada wako, aliendelea. "Pesa hizo zilizotolewa zitagawanywa miongoni mwa wavulana ili kusaidia kulipa baadhi ya bili zetu ambazo hazijalipwa."
Pamoja na kwamba timu hiyo bado ina kazi kubwa ya kujiandaa na mashindano yajayo, kwa mujibu wa Ambaka, wamelazimika kutafuta rasilimali zao na kutegemea watu wachache wenye mapenzi mema ndani na nje ya nchi kufidia gharama zao.
Timu imeanzisha nambari ya malipo ya MPesa 891300, Nambari ya Akaunti 60365, na kiungo cha MChanga ili kuwasaidia kutimiza maombi yao.