Timu ya raga ya shule ya upili ya Butula ya wachezaji 15 kila upande imepigwa marafuku kushiriki katika mashindano ya shule za upili ambayo yameandaliwa Uganda FEASSA.
Hii inajiri baada ya timu hiyo ya raga kuchezesha wachezaji wawili ambao si wanafunzi wa shule licha ya kuwa na wechezaji wa kutosha wa akiba.
Ni jambo la kufedhehesha kuona wachezaji waliojituma katika hatua ya zone,kukosa nafasi ya kuchezea timu ya shule yao na mwisho kupigwa marufuku katika michez hiyo ambayo inaendelea huko Uganda .
Ni jambo ambalo litakatiza ndoto la taifa la Kenya na kwaivyo kuwanyima nafasi ya kutamba.Vile vile wafuasi wengi wamejadili swala hilo kuwa na utovu wa nidhamu kwa kamati ya timu hiyo kuwa walikuwa wanajua yakakwamba ni jambo ambalo huenda likawagharimu pakubwa.
Aidha ,sio mara ya kwanza timu ya Kenya katika mashindano hayo kupigwa marufuku baada ya timu ya hapa nyumbani mwaka jana ,Koyonzo kupigwa marufuku kwa madai hayo tu.
Aidha ,sio mwisho wa timu za raga kutoka Kenya baada ya timu mbali mbali kutoka apa nyumbani kuzidi kufanya vyema kwa mfano timu za All saints Embu,Lenana school na pia vilevile Kitondo.
Kutokana na marufuku hayo sasa timu hiyo haitakuwa nauwezo wa kushiriki mashindano hayo mwa miaka 3 ,jambo ambalo ni igo kwa vipaji ibuka katika shule hiyo.