Mkondo wa mwisho wa Sportpesa National 7s wawadia

Prinsloo 7s kufanyika jijini Nakuru tarehe 14 na 15 Septemba

Muhtasari

• Mabingwa wa Driftwood 7s kuongoza kundi A pamoja na Menengai Oilers, Zetech na Mombasa RFC.

• Raga ya akina dada kujumuishwa kwa Prinsloo 7s wakati Kenya Lionesses wakijianda kumenyana na Madagascar Women mechi ya majaribio

Mchezaji wa Simba wa Kenya Isaac Njoroge akicheza dhidi ya Uganda katika mechi iliyopita ya Kombe la Elgon
Mchezaji wa Simba wa Kenya Isaac Njoroge akicheza dhidi ya Uganda katika mechi iliyopita ya Kombe la Elgon
Image: STAR

Msururu wa raga wa Sportpesa National 7s unaingia mkondo wa mwisho wikendi hii tarehe 14 na 15 katika uwanja wa riadha wa Nakuru jijini Nakuru.

Tayari timu zimegawanywa katika makundi husika kwa mashindano ya #Prinsloo 7s.

Timu za raga za upande wote wa kiume na kike zitamenyana wikendi hiyo kwenye shindano kuu na dirisha la pili.

Katika mashindano ya daraja la pili, Kundi la kwanza limebeba timu za raga za Tum Marines, Bungoma RFC, KCA University na Jackals.

Kundi B lina timu za NYS Spades, Mean Machine, Molo RFC na Rongai Marines.

AP Warriors, Nandi Bears, JKUAT na Kisii RFC watamenyana kwenye kundi C.

Kundi D litahusisha migwaruzano baina ya Ngong Warriors, Eldoret RFC, N. Suburbs na Presbyterian University.

Kundi la mwisho E lina MKU Thika, Homeboyz RFC, Project 61 na Kisii Kifaru wakipambana kufika hatua za mbele.

Miamba wa raga nchini Kenya Kabras Sugar, wanaongoza kundi D wakiwa na Daystar Falcons, Stallions Rugby na Kabarak University kwenye shindano kuu la raga nchini.

Kundi A lina Zetech University, Mombasa RFC, Menengai Oilers na mabingwa wa msururu uliopita wa Driftwood 7s Kenya Harlequin wakati kundi B likijumuisha KCB Rugby pamoja na Nondescripts, Mwamba RFC na Nakuru RFC.

Kundi C lina KU Blakblad, Strathyre Leos, MMUST na Catholic Monks.

Kwa upande wa wanadada, kundi A litaongozwa na Impala wakiwa na Ruck It, Western Spears na NYS Gilgil.

Kundi B litashuhudia mapambanao ya timu za Mwamba, Kenya Harlequin, Meru Ladies na Groundshakers. Kabarak University, N. Suburbs, Nakuru Ladies na NYS Spades watapambana ndani ya kundi D.

Timu ya taifa ya raga ya wanawake akenya Lionesses nao watacheza mechi ya kirafiki dhidi Madagascar Women tarehe 20 Septemba, 2024 katika uga wa RFUEA. Mchuano huu unafanyika takribani mwaka mmoja tangu timu hiyo kucheza mechi ya majaribio Novemba 2023 jijini Kisumu.