Visa ya nyota wa mchezo wa tenisi Novak Djokovic ya kuingia Australia ilibatilishwa alipowasili Melbourne.
Mchezaji huyo nambari moja duniani alishikiliwa katika uwanja wa ndege wa jiji hilo kwa saa kadhaa kabla ya vikosi vya mpakani kutangaza kuwa hajakidhi sheria za kuingia na atafukuzwa.
Inasemekana kuwa sasa amepelekwa katika hoteli ya kuzuilia watu ya serikali akisubiri kuondoka kwa ndege ya nje.
Matukio hayo yanakuja huku kukiwa na msukosuko kuhusu kutotozwa chanjo Djokovic alisema alistahili kucheza katika michuano ya wazi ya Australian Open.
Djokovic hajatoa tamko lolote kuhusiana na hali yake ya chanjo , lakini mwaka jana alisema kuwa "anapinga chanjo".
Tenisi Australia ilithibitisha msamaha wa kimatibabu kwa mchezaji huyo "kufuatia mchakato mkali wa ukaguzi unaohusisha majopo mawili tofauti" lakini matatizo yaliibuka baada ya Djokovic kuwasili Melbourne Jumatano jioni kutoka Dubai.
Katika taarifa, Jeshi la Mpakani la Australia lilisema Djokovic "alishindwa kutoa ushahidi ufaao ili kukidhi mahitaji ya kuingia Australia, na visa yake imefutwa.
Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison amekanusha kuwa Djokovic anatengwa na kusema hakuna mtu aliye juu ya sheria za nchi.
Katika mkutano na wanahabari siku ya Alhamisi, Bw Morrison alisema kuwa alishauriwa kuwa hakuna ruhusa ya matibabu kwa mchezaji huyo kuingia na kuongeza kwamba ushahidi uliotolewa "hautoshi".