Katika video moja ambayo imesambazwa pakubwa kwenye mtandao wa Instagram, inaonesha mchezaji mmoja wa tenisi akimzaba kofi moto mchezaji mwingine aliyemshinda katika mchezo huo.
Katika kile kinaonekana kaam maigizo ya kitendo cha muigizaji Will Smith akimzaba kofi mchekeshaji Chris Rock kwa kumdhihaki mkewe katika hafla ya tuzo za Oscars wiki mbili zilizopita, mchezaji huyo wa Ufaransa, Michael Kouame anamkaribia mwenzake wa Ghana Raphael Ankrah na kumzaba kofi la kushtukiza.
Runinga ya Fox iliripoti kwamba mchezaji huyo wa Ufaransa alichukizwa na uhalisia kwamba mchezaji wa Ghana ambaye ni mdogo kiumri alimshinda katika mchezo huo wa tenisi na kumuita kama vile anataka kumpa hongera lakini hongera yenyewe ikawa kofi la moto wa tanuru.
Mashindano hayo ya kimataifa ya mchezo wa tenisi yalikuwa yanafanyika katika mji mkuu wa Ghana ambapo baada ya mwenyeji kumchachafya mgeni katika raudni ya kwanza, mgeni alikosa heshima na kujiliwaza na kumzaba kofi mwenyeji wake.