Podi ya Yusuf Juma

Simu za mkononi zinavunja ndoa na mahusiano ya watu wengi+Podi ya Yusuf Juma

Simu zimekuwa chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano mengi

Muhtasari

 

  •  Iwapo katika ndoa hamfichani lolote au hakuna anayefanya mabaya huko nje ,hamna haja ya kuificha simu yako ili mwenzako asione jumbe
  • Hadi leo kuna visa vingi ambavyo marafiki ,jamaa katika familia na hata viongozi wa kidini wanapatanisha wana ndoa kuhusu mambo ya kuichukua simu ya mwenzio ili kutaja kujua yaliyomo 

 

 

Ni kifaa kidogo cha mkononi ambacho kilifaa kurahisisha mawasiliano  miongoni mwa watu . Lakini sasa iwapo kuna njia rahisi ya kuvunjika kwa ndiooa ama sababu  kubwa ya kuvunja mahusiano basi simu ya mkononi imetajwa kuwa nambari moja katika orodha hiyo

Simu za mkononi sasa zimekuwa kama sumu kwa mahusiano na ndoa .Ukiteleza ujipate umepitishamacho katika jumbe za simu za mwenzako basi utakuwa na bahati kuendelea katika uhusiano huo .

Wengi wanajutia au hata kufurahi kwa uamuzi wao wa kujipata wakchungulia jumbe na mawasiliano ya wenzao katika simu zao wa mkononi lakini jambo ambalo hawakulipangia ni matokeo yake .