Wivu katika mapenzi ni jambo la kawaida ,lakini utajuaje iwapo wivu wa mwenzako umevuka mipaka?
Amesimulia kisa kimoja jamaa ambaye mpenzi wake ana wivu kupindukia na kila hatua inayoonekana a kawaida kwake humtia mashakani .Hawezi hata kuwa na rafiki wa kike au kuamkuana na mtu wa kike wakicheka . Kesi zake mbele ya ‘mahakama’ ya mpenzi wake zinafanyika kila siku na sasa ameanza kujiuliza iwapo kuna tatizo Zaidi ya kinachoonekana kuwa wivu wa kimapenzi .
Katika Podi hii nzima tunajadili masaibu yake na kufahamu ni kiwango kipi cha wivu kinachofaa kuchukuliwa kama cha kawaida