Podcast

Uchambuzi wa hali ya kisiasa Nchini Kenya na uchaguzi uliokamilika nchini Uganda#PodiyaYusufJuma

Nchini Uganda Rais Museveni ameshinda uchaguzi kwa njia tata huku upinzani ukilalama kuhusu kukandamizwa

Muhtasari

  •  Hali itakuaje iwapo kweli rais  Uhuru hatamuunga mkono naibu  wake Ruto kama alivyomuahidi?
  •  Je,nchini Uganda  Bobi Wine atapata haki kupitia mahakama ambao majaji wake wanateuliwa na rais Museveni?

 Katika Podcast hii tunatathmini hali ya kisiasa nchini Kenya baada ya kuibuka makundi mawili kuhusu anayefaa kumrithi rais Uhuru kenyatta na pia tunaangazia kinachofuatia nchini Uganda baada ya Rais Yoweri Museveni kushinda hatamu ya sita kuongoza taifa hilo

 Maajuzi  rais Uhuru Kenyatta alijitokeza kutoa usemi ambao  uliwaacha wengi vinywa wazi  aliposema kwamba huenda wakati umewadia kwa taifa kuongozwa na  mtu kutoka kabila tofauti kando na jamii  za kikuyu na Kalenjin .