(+ Video) Harmonize a-copy paste Baba Lao ya Diamond Platnumz, video mpya

Staa wa Bongo Harmonize almaarufu kama Konde Boy ameachilia video ya wimbo wa Kushoto Kulia.

Video hii ina nembo ya lebo yake ya Konde Gang tofauti na kazi za awali zilizokuwa na nembo ya WCB.

WCB inayoongozwa na Diamond imemlea na kumkuza Harmonize.

Rayvanny adondosha Remix ya Tetema na mastaa wakubwa Afrika

 Audio ya Kushoto Kulia imefanywa na producer wawili Bonga huku video ikiongozwa na Hascan.

Idea au concept ya video inaonekana kufanana na ya Baba Lao ya Diamond Platnumz.

Katika video ya Harmonize, kuna sehemu na ambapo yupo katikati mwa watu waliojifunga buibui nyeusi.

Dakika 5 tu niage dunia, Msanii wa nyimbo za injili Roz Haki afunguka

Video ya Baba Lao ilitangulia kudondoka huku Diamond Platnumz akionekana kati ya watu waliovaa suti na kujifunga vitambaa vyeupe.

Ni juzi tu Harmonize alikuwa katika ubishi wa midundo ya UNO na mtayarishaji wa nyimbo Magix Enga almaarufu kama Beat King.

Magix Enga hatimaye alitangaza kumsamehe.

Akichapisha ujumbe kwenye Insta, Enga alitangaza kuwa walimaliza tofauti zao.

Kuna uwezekano pande mbili zilipatana baada ya ubishi kuwepo kuhusu mdundo wa ngoma hiyo.

 Katika video hiyo, Enga anasikika akiuliza maafisa hao “Mnanikamatia nini mazee kama wimbo ya Harmonize tayari iko YouTube.”

Yote tisa, concept ni ileile.

Sio mara ya kwanza Konde Boy kutuhumiwa kumuiga Diamond ata jinsi anavyoimba na kunengua katika video zake.

 

(+Video) Harmonize alivyomfurahisha Pombe Magufuli, dili na Wizkid

Nyota wa Bongo Fleva, Harmonize amewafurahisha maafisa za ngazi za juu serikalini kwa kuimba wimbo wa ‘Magufuli.’

Katika wimbo huu, Harmonize anamsifia rais huyo pamoja na miundomisingi iliyojengwa na serikali ya sasa.

Konde Boy alikuwa anatumbuiza mashabiki na kuwakonga nafsi katika sherehe za Nyerere Day nchini humo.

Zari The Boss Lady aifokea Kenya Airways, awaita wezi

Rais Pombe Magufuli hakusita kusimama na kusakata ngoma hii.

View this post on Instagram

I don't play around when it's come to my beautiful country Tanzania…!!!! I was there 2 represent all 🇹🇿 Youth thanks again Mr President Doctor John Pombe Magufuli my number one supporter I'm grateful 🙏🙏 lakini pia kipekee kabisa nimshukuru mheshimiwa P.M. Kassim Majaliwa Kassim kwakunipa molari na msisitizo nisipitwe na hili tukio ukizingatia sikuwa nchini Ila kwa uzito wa kauli yako na kuthamini uwepo wa Serikali yangu pendwa nilifanikiwa kuwahi …!!! bila kusahau mama yangu makamu wa Rais Mama Samia Suluhu nakushukuru sana Na ile bahasha imefanya siku yangu ikawa ya kipeke mno…!!! Pia shukrani za kipekee zikuende waziri mwenye dhamana Ya michezo sanaa burudani baba yetu Docter Harison Mwakyembe shukrani baba…!!!!! viongozi wote wa serikali mliosimama kwa ishara ya upendo na kupendezwa kile anachokifanya kijana wenu…!!! Mungu awabariki Sana….!!!! 🇹🇿🙏🙏….. #HappyBabaWaTaifaDay #HappyKileleChaUkimbizajiWaMwengeWaUhuru @Kondegang

A post shared by KONDEBOY (@harmonize_tz) on

Hii ni baada ya wimbo huu kuwapendeza wengi katika hafla hiyo.

Haya yanajiri huku staa huyu akitangaza kufanya collabo kubwa na msanii kutoka Nigeria, Wizkid.

Konde Boy tayari ashatangaza kuibadili Bongo Fleva iwe na jina la Afro East ambalo anadhani linaafiki muziki huu ambao unatamba kwa kasi.

Je, Mariam Kighenda alipanga kujitoa uhai? Mmewe John afunguka

Jeshi alihakiki collabo hii kupitia mtandao wake maridhawa wa Insta.

Hafla hii ya AfroEast lilifanyika kwa siku 2 miji ya Melbourne, Sydney na nchini jirani ya Tanzania.

Kama Jeshi atamshirikisha Wizkid katika ngoma, hii bila shaka inatazamiwa kuwa kubwa zaidi baada ya kolabo na Yemi Alade, Burna Boy, Timaya na wengineo.