Waziri mkuu wa Lesotho Dkt. Motsoahae Thomas Thabane kuzuru Kenya

Waziri Mkuu wa Lesotho Mheshimiwa Dkt. Motsoahae Thomas Thabane, atawasili humu nchini hii leo Jumapili tarehe 10 mwezi huu kwa ziara ya Kiserikali.

Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta atampokea rasmi Waziri Mkuu huyo katika Ikulu ya Nairobi mnamo siku ya Jumatatu tarehe 11 mwezi huu.

Baada ya sherehe za mapokezi, viongozi hao wawili watafanya mashauri ya faraghani kabla ya kuongoza jumbe zao kwa mashauriano kati ya nchi zao.

Mara tu watakapomaliza mashauriano, Rais Kenyatta na Waziri Mkuu Thabane watahutubia waandishi wa habari.

Hayo yakijiri, Polisi mjini Voi wanachunguza kisa ambapo mwanamume wa umri wa makamo amejitia kitanzi, mtaa wa Msambweni mjini Voi usiku wa kuamkia leo.

Mwanamume huyo ambaye wenyeji wamesema  ni mwashi,amepatikana mapema Leo akininginia kwa paa la nyumba yake.
Haijabainika kilichomshinikiza mwananmume huyo kujitoa uhai ,ila kwa sasa polisi ambao wamefika nakuuondoa mwili huo wamesema ripoti kamili itatolewa baada ya upasuaji.
-PSCU/ Solomon Muingi