Patanisho: Mke wangu hupigia customer wangu wa Uber na kubishana nao

Abel na Zippoteha walikosana juzi mwezi kama moja iliyopita baada ya mke wake kubadilika alipopata kazi

Wapendwa wawili hawa wamekaa miaka sita bila kukosana na Abel alituma SMS akiuliza apatanishwe na mke wake.

Huyu ndugu anasema mke wake alibadilika baada ya kupata kazi kule Mlolongo na alikuwa akimshugulikia pale wiki sita bila kulipwa na yeye alikuwa anafanya kazi ya Uber.

Anadai mke wake alianza kubadilika baada ya kwasababu wame ishi miaka sita hawakuwa wamewahi kosana.

‘Wanawake Kenya ni kama njugu’ shouts Pastor Deya on fighting temptations

Abel na Ziporrah wana watot wawili na anasema siku ya tukio kuan dada alimchungulia Facebook pale na sijui ni kama alificha simu sasa mke wake ni kama alikasirika akapigia dadake na kumweleza na dadake akapigia huyu jamaa ambaye alimweleza ni kwa nini unaficha ficha dadangu mambo hapa na pale eti huenda ikawa anamdanganya na mambo kama hayo. Kisha baadaye ndio akapanga na wakatoroka nyumbani. Abel akafuata akampelekea mtoto kwa njia alikuwa ameshawishiwa kwamba hiyo ndio njia itafanya mke wake arudi.

Lakini hadi wa leo mke wake hajarudi kwa hivyo angependa Redio Jambo imsaidie arudiane uhusiano.

Bi Zipporah hakuweza kushika simu na ikabidi wanajambo wampe mawaidha.

Je Abel anauhakika hajatongoza wanadada ambao anawabeba akiwa kazi ya Uber, ndio maana bib yake Zipporah amekasirika?

Alisema akiwa na huzuni’ Wacha nikwambie Gidi Mimi ndio mwoga hata kukiendaga hivo narudi namwabia tuende kwanza tupimwe sitaki kukufa ukimwi niache mali yangu ile nimetafuta.’ Sijawahi jaribu kutongoza msichana juu naogopa kukufa.Hapana mimi ni mwoga sana 

Kuna majirani walikuwa wanambia eti dereva wa taxi ni wabaya na mi namwambia hujanipata na msichana hata siku moja.

Na hii Facebook ambayo alikuwa nanamfichia ambayo ilileta vita, kwa nini alifanya hivo?

Abel alisema, ‘sikumficha ni simu yangu nilimwabia wakati nilipata message ya client amepiga simu nikiwa kwa bafu amechukuwa simu ametukana client juu ilikuwa Decemba 25 niklmwambia kuna kazi wacha niende. Niliendaa 25 mpaka 26 nikarudi na Sh30,000 na namwekea kwa meza’.

Also read more here

Patanisho: Nilimpata Bibi yangu akitongoza ‘cousin’ yake kwa bedroom

Mambo mengi ambayo ameptia pale kwa ndoa yamemsababisha bwana Fredrick apate depression.

Katika Patanisho hivi leo, tulisikia masaibu ambayo huyu ndugu alipitia katika ndoa lakini bado anampenda bibi yake Catherine, na angependa warudiane lakini inaonekana kwamba mke wake hayuko tayari kuzungumza.

Kwanzia 2015 bwana Fredrick hajweza kuona watot wake kulingana na maelezo yake kupita kitengo cha patanisho.

Nini ilisambaratish ndoa ya Fredrick na Catherine?

‘Bib yangu alikuwa na mpango wa kando nikagundua, alisema Fredrick.

Nikajaribu kuhepa hepa kama mwanaume, lakini ilibidi tuwachane because of that Ilianza 2014 by the way mimi nilikuwa nafanya kazi nyumbani huko Homabay na yeye alikuw Nairobi so mos t of the time nilikuwa naenda kumtebelea over the weekend nikimaliza kazi. Kuna siku tuu nilimpata  na kijana mwingine kwa nyumba yangu nikamuuliza huyu ni nani?

Akaniambia huyu kijana ni rafiki yake wanafanya kazi pampoja, so kidogo kidogo nikamuuliza it’s not bad ukiwa na rafiki lakini most of the time namwonanga anakuja hapa anatsfuta nini? 

Akaniambia ah!1 usiniulize mambo mengi. huyo ni rafiki yangu na hiyo mambo iishe. 

Aliibua aje huyo kijana rafiki wa mke ni mpango wa kando?

So kuna siku kuna jirani amenipigia simu akaniambia hiyo nyumba yako itaharibika. Kuna kijana anakujanga hapa mst fo the time ukiwa away ebu fanya uchunguzi. So siku yenye tuliwapata ni day nilijifanya sitakuja weekend, akaniambia sawa wewe jipange.

So kisiri nilipanda gari, kufika Nairobi saa kumi na moja kugonga gonga mlango hakuna mwenye ananifungulia. So housegirl ndio alitokea akaniambia mama bado analala. Kidogo kidogo kwenda kwa balcony hivi naona mwenye anatoka kwa bedroom yangu Nikaona kijana ametoka kwa bedroom akanisalimia! Doh 

Catherine alipata mshtuko wakti Gidi kutoka Radio Jambo almpigia simu kumpatanisha baad ya bwanake Fredrick kuomba patanisho kwasababu ya mapenzi.

Kisa na maana?

Catherine hauwa anashika simu kwa mara ya tatu na ikabidi Gidi kumpatia bwana Fredrick ushauri kwasababu alionekana amesononeka sana.

Huku amjezwa na majonzi, bwana Fredrick. alianza kulia.

Gidi alimhimiza Fredrick kwamaba inaonekana kwamba Catheire hataki kuongea, na kumwambia kwamba kisheria anaweza kuona watoto kuptiia uamuzi.

Huenda kuna wengi wamepitia masaibu kama yake na wanaweza mpatia ushauri?

Skiza kanda ifuatayo

Patanisho: Bwanangu alisave picha ya mpango wa kando kama screensaver

 

Bwana Okumu na bi Tecla waliachana baada ya bibi kutoroka mwezi wa pili mwaka huu. Kisa na maana? Tecla aliibua kwamba Okumu alienda kulala nje siku kadhaa Tecla akakasirika.

Okumu alieleza:

bwana Ghost bana nimepitia changamoto mingi. Mimi nimekaa na bibi yangu miaka nne, na bibi yangu anilimuoa akiwa na mtoto wa mtu mwingine. alijifungua akiwa shule, na nikaona kuliko akae kwa boma, nikamuoa nikampeleka nyumbani, tukapata mtoto msichana.

kukaa hivi tukaanza mambo ya nyumba tukaanza kusumbuana na mwishowe akaniibia vitu zangu akatoroka nyumbani Februari mwaka huu.

Sasa aliniibia mabati zangu na kuku, kila kitu yani maisha ikaanza zero tena. Nilikuwa nime enda kazi.

Je alikuwa wapi bibi yake kaiiba?

Nilikuwa nimeamka asubuhi nimeenda kazi. ati alinishuku niko na mpango wa kando

Je amekubali hayp mashtaka?

Eh nimekubali nilukuwa na mpango wa kando.

Sasa hivi tukuongea, mke wake ako wapi?

naiskia ako upande wa Nyahururu Laikipia na anafanya huko kazi alipotoroka aliwaachia sister yake mtoto huko nyumbani na huyo mtoto aliwachwa side ya Webuye. 

Hakuniwacha na mtoto alitoroka na mtoto pia. 

Tangiye wameongea?

Karibu siku mbili iliyopita, anasema ningoje mpaka Decemba anasema tuu tutarudi pamoja na baba yake mpaka amenipigia simu akisema nikae na mtoto wake tuongee nimkalishe chini.

Ghost alipigia Bi Tecla simu ambaye alisema

‘Okumu alikuwa anaenda nje na alikuwa akisema mimi sio bibi yake. Ati bibi  yake ni Purity. Aliweka picha ya Purity kwa screen ya simu aliniandikia barua akasema mimi siyo bibi yake, bali ni Purity. Aliandika akaniwachai kwa meza. 

Tecla akakta simu, na mawasiliano yakaisha hapo baada ya Bi Tecla kukaasirishwa na maneno ya Bi Purity na yeye mwoyo wake bado anasononeka.

Skiza kanda ifuatayo

 

Patanisho: Jombi aapa kutopiga bibi yake

Edwin, 32, alipiga simu katika kipindi kinachoruka kinachopendwa na watu wengi kila asubuhi katika redio Jambo cha Patanisho kupata suluhu la takribani miezi tatu kufikia sasa. Bwana huyu alisimulia mwanzo mwisho masaibu yaliyoikumba ndoa yake ya miaka kumi na mwili. Balaa iligumbika na kuyafanya mapenzi yake kuwa shubiri kuanzia mwezi wa kwanza alipompiga mpenzi wake Christine.

Kupitia kwa njia ya kupiga simu redioni jombi huyu alionekana kusononeka sana na kuyakubali makosa yake ya kumpiga na kumdhalilisha mkewe kadamnasi ya watu “…Makosa yalitokea lakini najuta sana.Am the one who messed up… nilipiga bibi akaenda Am missing my family… mimi ndo nilijiletea shida mwenyewe.”

PATANISHO: Mume wangu hutaka tufanye mapenzi hadi nikiwa na periods

Baada ya kuipoteza kazi yake iliyomletea fedha za kuisetiri familia yake. Edwin alianza kupandwa na hasira za mkizi na kuanza kuivuruga familia yake kila mara. Alikuja nyumbani siku moja na kuchukua simu ya mke wake na kuanza kuipekua katika kasha la jumbe.Ujumbe aliokutana nao ukiwa wa mwanaume mteja wake Chrisine.

Baada ya mtangazaji aliyobobea katika taaluma hii Gidi kumpigia mke wake, mama huyu wa watoto wawili alionekana kutotaka kurudi katika ndoa ya vita kila mara. Alifunguka zaidi jinsi bwana huyu anawatesa yeye na watoto “Amekuwa ananifukuza kwa nyumba, kunipiga pamoja na watoto mara anatupa anatupa vitu nje ya nyumba.”

Kwa majonzi zaidi amesimulia jinsi na ambavyo ndoa hii ya miaka kumi na miwili ilikumbwa na tandabelua na zogo tele. Bibi huyu alihoji kuwa jumbe zilizokuwa katika simu zilikuwa za mteja wake wa kiume na walikosana na bwanake. ”Huyo mtu alimtext nasty words na kuanza kunipiga mbele ya mamake…ata mbele ya wazazi wake wote”

PATANISHO: Sina wanawake wengine hao ni ma customers!

Christine alifunguka jinsi bwanake anamshuku kila mara na wanaume na ata kufikia kiwango cha kuwakana watoto .“Unasema watoto si wako… you almost killed me mbele ya watu wengi .Give me time …” alifoka Christine.

Bibi yake amesema yupo radhi kurejea katika ule uhusiano iwapo atabadilika na kuasi tabia za kinyama na kumdhalilisha. ” If I hear changes from people I will come back.”

Patanisho hii ilifikia kikomo na Gidi kumtaka Edwin kula kiapo kwa kuinua mkono wake wa kulia “..Mimi Edwin Odero naapa ya kwamba sitarudia tena kumpiga mke wangu mama Beverly, kumwaibisha mbele ya familia na nitampenda kuanzia leo hadi kifo kitutenganishe Amina”

Patanisho: Niliharibu ndoa ya kijana wangu baada ya kuenda kwa mganga

Ni miaka kumi tangu huyu baba na kijana wake wawasiliane.

Kisa na maana?

Alienda kwa mganga ampatie dawa aweke kwa chakula lakini huyo kijana akagundua.

Bwana  John alimwelezea Gidi kwa ufupi

 ‘tumekosana for so many years, sasa katika hiyo harakati ya kujaribu angalau tuongee na yeye imenishinda so rafiki yangu akaniambia tumia njia ingine akanielekeza kwa mganga. Nikatoa hiyo dawa nikapea bib ya kijana wangu. Unajua sasa lazima utafute mtu akokaribu na yeye nikampea akajaribu kumwekea na kijana akanotice. Sasa hiyo ikafanya tukakosana. 

Mzee amesononeka sana kwasababu huyo kijana wamekosana na bibi yake.

‘Ehe aligundua niliambia bibi yake aweke dawa kwa chakula yake’ aliongeza Mzee John.

Na hii dawa ingechangia nini?

Ni ile tuu niliambiwa eti itaweza kumbadilisha kwa njia moja iweze kubadilisha na aweze kurudi nyumbani. 

Na walikuwa wamekosana na huyo kijana?

Mama yake alikufa sasa nikaoa mke mwingine. Kuoa mwingine sasa ndio wakakosana yani pia yeye alijaribu kumwuua. hawakuwa wanaskizana.’

Mbona ma wa kambo alikuwa anataka kumwuua huyu kijana?

John alisema, ‘ Alijaribu kabisa akamwekea dawa na si mara moja na kijana alikuwa akiwekwewa. Sasa kuna vile sikjui kijana alijua vipi, sasa akatoroka nyumbani na kasema hatawahi rudi’.

Alihimiza Gidi aweze kumpigia simu kijana wake, washirikiane huku akisema’

unajua kunawakati tulijaribu kuskizana na yeye lakini kwa vile alikuwa tumejaribu kumwuua akaniambia kama unataka mtu aahidi mali yako basi nenda ukanunua mtoto. Sasa tafadhali hiyo imenichanganya lakini hata hivyo nilimpita mpaka kuharibu ndoa yake 

Doh!

Mke wake kwa sasa alifukuzwa nyumbani na mvulana anayeitwa Mike.

Kwa bahati mbaya Gidi hakuweza kumpata Mike kupitia simu na wakaamuua wapigie bibi ya kijana.

 

 

 

PATANISHO: Ndugu wa toka nitoke wagombana vikali hewani

Bwana Elkana alituma ujumbe akiomba apatanishwe na nduguye Obed akidai kuwa alitoa madai ya kwamba aliua baba yao na tena anapanga kumuua ili abaki na shamba lao.

Alipopigiwa simu bwana Obed alidai kuwa hataki kuskia maneno ya nduguye mdogo kwani yeye huwa hasaidi familia yake ila yeye huchangiwa mke wake akiwa mgonjwa.

“Nilimpigia simu nikamwambia kuwa ndugu yako amekuwa mgonjwa sana na inafaa tumsaidie tumpeleke hospitalini.” Alieleza kabla ya kumwambia nduguye kuwa hataki wawili hao waitane ‘ndugu’.

Wawili hao walianza kugombana sana hewani naye Elkana akadai kuwa yuko tayari kuuza mali yake ili ahame na kuondokea matatizo hayo yote. Isitoshe alidai hataki kutambulika kama ndugu yao.

Pata uhondo kamili.

 

PATANISHO: Mimi nataka Lucy, huyo mwanamke mwingine ni expensive!

Bwana Achimba alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Lucy ambaye walikosana mwaka wa 2016.

Patanisho: Evans alimfumania mke wake kitandani mwao na jamaa flani (AUDIO)

“Huwa tunazungumza naye lakini hatujazungumza kuhusu mambo ya kurudiana ila ni mambo ya watoto.

Tulikosana baada yake kuanza madharau na nikakasirika nikavunja simu yake. Isitoshe nilikuwa na tabia za kunywa pombe na kuwa na mipango za kando.” Alieleza Achimba.

Alipopigiwa simu bi Lucy alidai anamfahamu Achimba kama baba wa watoto wao.

“Sasa tuaongalie watoto aje na ulibeba mtoto mmoja? Kama unataka tuzungumze chochote unirudishie mtoto.” Aliuliza Lucy akidai kuwa bwanake ana bibi na hana kwa kurudi.

Imagine alikuja akachukua mtoto nyumbani akiwa mchafu nyumbani na nimejaribu kumwambia amrudishe nashindwa. Isitoshe ana bibi na am very sure.” Aliongeza.

PATANISHO: Sitaki mume wangu apate kitambi afanane na tank ya maji

Bwana Achimba alifichua kuwa baada ya kuwachana na Lucy alitafuta mke mwingine ambaye alikuwa anaishi kwake, lakini mtoto wake hakuwa anampenda na pia mamake Achimba hakumkubali.

“Huyo mwanamke ni expensive sana, unajua Lucy ukimuachia elfu moja unajua utakula lakini yule mwingine ukimuachia fedha bado ataitisha za maziwa.” Alisema.

Pata uhondo kamili.

Mke wangu alitaka kunidunga na kisu alipogunuda nina mpango wa kando

Obadiah alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe ambaye wameoana kwa miaka minane. Alidai mkewe Grace walikosania swala la mpango wa kando.

PATANISHO: Bwanangu huniona kama mbwa kwa nyumba

“Ilikuwa kitu June tarehe 11 wakati mke wangu aligundua nina mpango wa kando. Huyo msichana alikuwa rafiki wa Grace wa ndani kabisa na pia akawa rafiki wa familia. Tulikuwa tunashinda naye na akaja akajua siri za familia yetu zote na tukikosana na bibi kidogo anajua.

Sasa akachukua hiyo nafasi tukaingiana naye, kitu kama mwezi wa nne mimi naye tukawa karibu kabisa na kufikia June tukaanza urafiki.

PATANISHO: Bwanangu aligeuka kuwa deadbeat

Bibi alijua na akaondoka mara ya kwanza lakini tukazungumza na akarudi, Jumapili moja bibi alianza kurudi kwenda kumuuliza shida ni gani akaanza kulia na kudai kuwa nilikuwa nimetoka kwa Reginah.” Alieleza Obadiah.